Ticker

6/recent/ticker-posts

FETA YATAKIWA KUTANUA WIGO WA MASHIRIKIANO KATIKA KUTOA MAFUNZO

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) imetakiwa kuongeza wigo wa mashirikiano katika kutoe elimu ya uvuvi.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Shekh wakati akifunga mafunzo ya siku 30 ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchini Somaliland, mafunzo ambayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Prof. Shekh amesema kuwa FETA inatakiwa kuongeza wigo wa mashirikiano na nchi mbalimbali kwani zipo rasilimali nyingi na wataalam wapo wa kutosha hivyo haitakiwi wataalam kujifungia wenyewe badala yake wajitokeze na kuhakikisha wanatoa mafunzo ili kuongeza utaalam kwenye utekelezaji wa shughuli za uvuvi.

Vilevile amewasihi kuendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo kwa watu wa ndani na nje ya nchi hasa wanaijishughulisha na shughuli za uvuvi.

Wataalam wa uvuvi kutoka Somaliland wamekuwa wakishiriki mafunzo hayo hapa nchini kwa lengo la kuongeza uwezo katika kusimamia rasilimali za uvuvi na kuhakikisha kuwa kuna kuwa na uvuvi endelevu nchini kwao.

Prof. Shekh amesema upo umuhimu mkubwa katika kuhakikisha mazao ya bahari yanakuwa na ubora unaotakiwa, hivyo ameitaka FETA kuhakikisha inaendela kuhamasisha na kutoa mafunzo hayo kwa washiriki kutoka nchi mbalimbali.

Vilevile amelishukuru Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ambapo ameyaomba na mashirika mengine kuiga mfano huo ili kuwezesha mafunzo hayo kuwafikia washiriki wengi zaidi.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Dkt. Semvua Mzighani amesema kuwa mafunzo yanayotolewa chuoni hapo msisitizo mkubwa huwa ni kwenye kufanya mafunzo kwa vitendo hivyo ni matarajio yake kuwa watakaporejea nchini kwao watakwenda kutekeleza yale waliyofundishwa kwa vitendo kitu ambacho kitawaongezea ujuzi zaidi na kusaidia kutoa elimu kwa wengine.

Vyuo vya vyao vinatoa mafunzo ya uhandisi katika maji, ubora wa samaki, uvuvi na ubaharia, ukuzaji viumbe maji, mazingira na rasilimali za bahari, sayansi ya bahari na menejimenti ya bahari.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wengine Rais wa wanafunzi hao kutoka chuo cha Uvuvi nchini Somaliland Bwana Elm A. Mohamed alisema kuwa nchi zetu vyema zikashirikiana katika rasilimali zetu kwani zinafanana hasa ukanda wa bahari pamoja na ufugaji vilevile tushirikiane kati Nyanja za utamaduni kwani utamaduni wa watanzania ni mzuri sana.

Mafunzo hayo ya mwezi mmoja yameanza tarehe 12/05/2023 na kumalizika tarehe 13/06/2023 ambapo pamoja na mafunzo washiriki wamepata fursa ya kujifunza Kiswahili na Tamaduni za Kitanzania.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchi ya Somaliland yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Prof. Sheikh amewataka washiriki kuyatumia mafunzo hayo katika kuongeza tija kwenye Sekta ya Uvuvi. (13.06.2023)
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Dkt Semvua Mzighani akitoa neno la utangulizi wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao ya Samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchi ya Somaliland yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Dkt. Mzighani amewasihi washiriki wa mafunzo kutumia vitendo zaidi katika kuyatekeleza mafunzo waliyopatiwa ili kuongeza ujuzi zaidi na kutoa elimu kwa wengine. (13.06.2023)

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh akikabidhiwa bendera ya Nchi ya Somaliland kutoka kwa Bi. Ubah Mohamed wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchi ya Somaliland yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani (13.06.2023)
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohamed Sheikh akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo kwa Arsar Aden mara baada ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchi ya Somaliland yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani. (13.06.2023)
Washiriki wa mafunzo kutoka nchini Somaliland pamoja na baadhi ya watumishi wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi iliyosomwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh (hayuo pichani). Mafunzo hayo yamefanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani. (13.06.2023)
Mwakilishi wa washiriki wa mafunzo kutoka nchini ya Somaliland Bw. Abubakar Adam akisoma risala kabla ya kufungwa kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakaguzi wa mazao ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchi ya Somaliland yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani (13.06.2023)
Picha ya pamoja kati ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohamed Shekhe (katikati) na washiriki waliohitimu mafunzo ya kuwajengewa uwezo wakaguzi wa mazao ya samaki juu ya usalama, ubora na taratibu za ukaguzi kutoka nchi ya Somaliland yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi kilichopo chini ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya uvuvi (FETA) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa pwani Juni 13, 2023.

Post a Comment

0 Comments