Ticker

6/recent/ticker-posts

MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI TANGA AKUTWA KANYONGA STOO


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

WATU wawili wamefariki dunia mkoani Tanga katika matukio tofauti likiwepo la mfanyabiashara maarufu jijini Tanga kukutwa amejinyonga na dereva wa bodaboda kuuwawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe amesema tukio la kwanza, mfanyabiashara Hamisi Rashid (53) mkazi wa Makorora, usiku wa kuamkia leo juni 27, amekutwa amejinyonga nyumbani kwake (stoo) kwa kutumia waya wa baada ya kujaribu mara mbili kujinyonga na kamba na kukatika.

"Taarifa hiyo tumeipokea kutoka kwa mke make wake Mwanaidi Issa lakini chanzo cha mpaka mareham anaemia kujitoa uhai hakijajukana, bado tuko kwenye uchunguzi" amesema Kamanda Mwaibambe.

Tukio la pili amesema kijana mwendesha bodaboda Damian Pius (24) mkazi wa Kongwa, Amboni amekutwa amefariki leo asubuhi katika barabara kuu ya Horohoro, eneo la daraja la Uto ofu ambapo amekutwa na jeraha kichwani baada ya kupigwa nakitu chenye ncha kali.

"Katika tukio hili tumemkamata mtuhumiwa mmoja, kwa majina Oscar Haule (26) ambaye pia ni bodaboda, kwa uchunguzi, kwa mujibu wa mashuhuda wetu wamedai eneo la tukio walikuwepo watatu baada ya mwenzao kuanguka walianza kugombania mirungi ambayo ilihifadhiwa katikati ya gonia la mkaa" amesema.

"Nitoe wito kwa wananchi, kutoruhusu jambo gumu likutawale mpaka kufikia hatua ya kujinyonga badala yake washirikishe watu wa karibu yao kwa ushauri zaidi, lakini pia waache kujichukulia sheria mikononi" amesisitiza Mwaibambe.

Post a Comment

0 Comments