***************
Na Hamida Kamchalla, TANGA.
MWENGE wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa kesho juni 9 katika uwanja wa ndege jijini Tanga ukitokea Wilaya ya Kusini Pemba, nchini Zanzibar.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amesema baada ya kupkelewa mwenge huo utakabidhiwa kwa mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa tayari kwa kuanza ziara ya kukagu na kuzindua miradi ya maendeleo kabla ya kukabidhiwa mkoani Kilimanjaro juni 20, 2023.
"Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika halmashauri zote 11 za Mkoa wa Tanga, umbali wa km 1,959 na utakagua, utafungua, utazindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 82 yenye zaidi ya thamani ya sh bil 25.9" amesema.
Aidha amebainisha kuwa ujumbe wa mbio za mwenge mwaka 2023, unahusu mabadiliko ya tabia nchi, hifadhi ya mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji, "hii ikon chini ya kaulimbiu isemayo, tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa" amesema.
Kindamba amesema mwenge utaendelea kuhamasisha na kuelimisha wananchi juu ya mapambano dhidi ya rushwa, malaria, Vvu na ukimwi, dawa za kulevya na uzingatiaji wa lishe bora.
"Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuulaki katika maeneo ya mapokezi, barabarani, kwenye miradi na maeneo ya mikesha" amesisitiza.
0 Comments