Ticker

6/recent/ticker-posts

NEMC, JMAT WAANDAA KONGAMANO LA KUJENGA UELEWA KUHUSU ATHARI ZITOKANAZO NA SAUTI KWENYE NYUMBA ZA IBADA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) wameandaa kongamano la Kitaifa la kujenga uelewa kuhusu athari zitokanazo na sauti zilizozidi viwango katika nyumba za ibada litakalofanyikaJuni 12,2023 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Juni 8,2023 Mwenyekiti Taifa -Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Dkt.Alhad Issa Salum amesema katika Kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa hivyo amewataka viongozi wa wote wa dini na madhehebu yote kuhudhuria ili kuweza kupata fursa ya kuelewa na uelewa wa hizo athari zitokanazo na sauti zilizozidi viwango.

Amesema kongamano hilolitawajengea uelewa zaidi katika lile linalokusudiwa na kupelekea waumini na wananchi wote kuishi kwa amani na utulivu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu NEMC, Dkt.Samuel Gwamaka amesema kwa kipindi hiki wamewalenga hasa viongozi wa dini pamoja na viongozi wa kimila hivyo amewataka wafiike wakiwa na vitambulisho vyao kwani wanahitaji kuwapatia elimu hasa wale ambao wamewakusudia.

"Tunaamini kwamba kwa kutoa elimu hii inayohusiana na suala la mazingira katika maeneo mbalimbali yanayogusa jamii hasa kwenye masuala ya kiafya viongozi hawa watakuwa mabalozi wazuri kufikisha elimu hiyo kwa wale ambao wanawalea katika nidhamu". Amesema Dkt.Gwamaka.

Post a Comment

0 Comments