Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ameongoza Menejimenti ya Wizara pamoja na wawakilishi wa JICA (Wakala wa ushirikiano wa Kimataifa Japan) , kujadili suala la uendeshaji na usimamizi wa Fursa na Vikwazo vya Maendeleo.
Kikao hicho kilichofanyika leo Juni 06, 2023 katika Ofisi za Wizara kinalenga kutafuta namna ya kuboresha uendeshaji na usimamizi wa Mfumo ili kuchechemua kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa jamii.
0 Comments