Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YATAKA WASHAURI WA WANAFUNZI KUWAJENGA WANAFUNZI KATIKA MAADILI MEMA NA UZALENDO


Mkuu waWilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Ushauri na Uelekezi kwa Washauri wa Wanafunzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TACOGA 1984), baada ya kufunga mafunzo yaliyohusu namna bora ya kukuza utendaji katika kuwapa ushauri wanafunzi yalioanza Juni, 21, 2023 na kufikia tamati Juni 23,2023 katika Ukumbi wa TIA Kampasi ya Singida.

..................................................Na Dotto Mwaibale, Singida

SERIKALI imewataka washauri wa wanafunzi na viongozi wa serikali za wanafunzi kuendelea kuwajenga wanafunzi katika maadili mema na uzalendo, umoja wa kitaifa ili wawe wabunifu ndani ya mazingira ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amesema hayo Juni 23, 2023 wakati wa kufunga mafunzo ya washauri wa wanafunzi na viongozi wa serikali za wanafuzi yaliyoandaliwa na Chama cha Ushauri na Uelekezi kwa Washauri wa Wanafunzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TACOGA 1984) ambayo ilisomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson.

“Ninyi washauri wa wanafunzi ndio mtakaoweza kuleta mabadiliko, nawaomba muendelee kuwajenga wanafunzi katika maadili mema na uzalendo, umoja na utaifa, nanyi viongozi wa wanafunzi shirikianeni vizuri na washauri wenu ili msaidie kuokoa maisha ya wenzenu,’’ alisema.

Apson aliwaomba washauri hao waendelee kuwashauri wanafunzi ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha wanasoma katika mazingira mazuri na kupatiwa misaada stahiki kama vile mikopo kutoka Bodi ya Mikopo HESLB na ZHELB.

Alisema jitihada ziongezwe katika kuwaelekeza kushiriki kikamilifu katika ukuzaji na uendelezaji wa vipaji na taaluma kwa lengo la kuimarisha moyo wa uvumbuzi miongoni mwa jamii ya vijana wasomi ili waweze kujitegemea baadaye.

“Waelekezeni kukuza uhusiano na ushirikiano baina ya Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Kati, Vyuo vya Ufundi pamoja na Taasisi za hiari zinazojishughulisha na masuala ya elimu, sayansi, tamaduni na maadili ya kitanzania, ili kuondokana na tabia za kuiga na kujiingiza kwenye masuala ya ushoga, madawa ya kulevya na bhangi,” alisema.

Aidha, aliwataka washauri watumieni na kuwashirikisha wanafunzi kufanya tafiti zinazohusu changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kupata usahihi wa yale yanayowasumbua zaidi na hatimaye kuyakabili kwa urahisi.

“Niwashauri muendelee kutumia mbinu za kisomi na kisayansi ili TACOGA1984 ije ijulikane kama ‘Association’ ya wataalamu na wabobevu wa masuala ya ushauri nasaha (ASSOCIATION OF PROFESSIONAL COUNSELLORS),” alisema.

Mwenyekitiwa TACOGA1984, Bi Sophia Nchimbi, alisema chama hicho kilianzishwa rasmi mwaka 1984 na kuwa vyuo vilivyoshiriki kwenye mafunzo hayo ni 39 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema kati ya kazi ambazo wanazifanya ni kutoa ushauri na unasihi katika ofisi zao na nje wadau wao wakubwa wakiwa ni wanafunzi, wafanyakazi na wengine kutoka nje ya ofisi zao na pia wanatoa mafunzo ya namna hiyo kwa Serikali za wanafunzi wa vyuo binafsi na shule za sekondari na kuwafundisha shughuli za mapambano ya kutokomeza ukatili.

Alitaja kazi nyingine wanazozifanya ni kufanya utafiti na pindi wanapokutana katika mikutano yao ya kila mwaka huwa wanabadilishana uzoefu kwani mara nyingi wanapoifanya peke yao inakuwa ngumu.

Alisema mafunzo yaliyotolewa ni kudhibiti migogoro ya wanafunzi katika vyuo, uongozi wa wanafunzi na usimamizi wa mabadiliko, ukatili wa kijinsia, kupunguza ukeketaji wa kijinsia vyuoni na kwa wanafunzi kwa ujumla, matatizo ya afya ya akili, ustawi miongoni mwa wanafunzi, VVU na Ukimwi na masuala mtambuka, usimamizi wa fedha za wanafunzi, bajeti, utunzaji wa fedha na ukaguzi, huduma kwa wateja, umuhimu, majukumu changamoto, pamoja na kusimamia na kuboresha miongozo ya ushauri nasaha.

Alisema pamoja na kazi hizo nzuri wanazozifanya kunachangamoto kadhaa zikiwemo za ushiriki mdogo wa wadau wao na vyuo kutoka wizara ya elimu, vyuo vya kati na vyuo vya VETA ambapo wakizungumza nao moja kwa moja wanataka kwanza wazungumze na wizara husika kwa ajili ya kupata kibali.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, ambapo yamefanyika mafunzo hayo Dk. James Mrema alishukuru ushirikiano uliopo baina ya TACOGA na TIA na akaomba udumishwe kwani wote wanajenga nyumba moja hawapaswi kuwa na utengano.

Dk. Mrema alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya juu kwani imewafanya wanafunzi wengi kuendelea na masomo ukilinganisha na siku za nyuma.

Mshauri wa Wanafunzi wa Sheria kutoka Chuo cha Sheria Zanzibar, Bi. Sabra Balyan Suheil akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo alisema yamewapa mwanga wa vitu vingi ambavyo walikuwa hawavijui hasa namna ya kumuhudumia mteja ambapo sasa wamepata mbinu hata za kwenda kuwahudumia waume zao na jamii kwa ujumla.

Mwenyekiti wa TACOGA 1984, Bi. Sophia Nchimbi ambaye pia ni Mshauri wa Wanafunzi (OUT), akitoa taarifa ya chama hicho wakati wa kufunga mafunzo hayo.Makamu Mwenyekiti TACOGA 1984, Ndugu Augustine Matemu, akizungumza wakati wakufunga mafunzo hayo


Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Dk.James Mrema (katikati waliokaa), ambaye alimuwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi hiyo, Tanzania, Profesa William Pallangyo akizungumza wakati wakufunga mafunzo hayo.


Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa katika ufungaji wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson, akimkabidhi cheti, Naibu Mshauri wa Wanafunzi MUDCC na Katibu Mwenezi wa TACOGA 1984, Bi Zitta Victoria Mnyanyi, Mshauri wa Wanafunzi wa Sheria kutoka Chuo cha Sheria Zanzibar, Bi. Sabra Balyan Suheil akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakibadilishana mawazo wakati wa ufungaji wa mafunzo.

Mafunzo yakifungwa.

Mafunzo yakifungwa.


Mafunzo hayo yakifungwa.

Furaha ikitamalaki wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.Washiriki wakiwa kwenye hafla ya kufunga mafuzo hayo

Mafunzo hayo yakifungwa.

Mafunzo yakifungwa.

Mafunzo ya siku tatu yakifungwa.

Taswira ya ufungaji wa mafunzo hayo.

Mlezi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar, Mhandisi Saad Hassan ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa TACOGA 1984 (kulia) akiwa na Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha KCMUCo na Mjumbe wa TACOGA 1984, Anza-Amen Lema wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.

Mwangalizi wa Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Kampasi ya Singida, Madamu Ambwene Kajula (kushoto) akikabidhiwa chti na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa katika ufungaji wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson.

Mhazini wa TACOGA, Bi. Ruth Kitundu, Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha MUHAS, akikabidhiwa cheti na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson.

Picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi

Picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Post a Comment

0 Comments