Ticker

6/recent/ticker-posts

TASAC YATOA WITO KWA WASAFIRI WANAOTUMIA VYOMBO VYA MAJINI

Afisa Mfawidhi wa Shirika la TASAC Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua akizungumza na vyombo vya habari katika Banda lao kwenye maoanyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Mfawidhi wa Shirika la TASAC Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara Conrad Millinga wa kwanza (kulia)ambaye alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo kuhusu namna ya kutumia vifaa vya kujiokolea wakati alipotembelea banda la TASAC katika maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin (kushoto) akimkabidhi zawadi Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara Conrad Millinga kulia wakati alipotembelea Banda lao

Na Oscar Assenga,TANGA


SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa wito kwa wasafiri wanaotumia vyombo vya Usafiri majini kuhakikisha wanatumia vyombo vilivyo ruhusiwa kisheria kubeba abiria na sio kupanda vyombo vya kusafirisha mizigo ikiwemo majahazi.


Wito huo ulitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga Kapten Christopher Shalua wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako Jijini Tanga


Aidha, alisema kwa sababu viwango vya vyombo vipo kwenye madaraja tofauti ni vema kila chombo kikatumika kulingana na matumizi huzika yaliyothibitishwa na amewataka wananchi wa Tanga kwa ujumla kutembelea Banda lao ili kupata elimu zaidi.


Alisema TASAC imeshiriki maonesho hayo kwa ajili ya kuwafikia wananchi hususani wanaoishi maeneo ya fukwe na kuwaelimisha kuhusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira Majini pamoja na majukumu yanayotekelezwa na Shirika hilo kwa Mujibu wa Sheria.


Hata hivyo alisema kwamba jukumu lao pia ni kuhakikisha wanasimamia Bandari kuhakikisha wanatoa huduma katika viwango vinavyokubalika kimataifa ili kuweza kuchochea ukuaji wa uchumi nchini .

Post a Comment

0 Comments