Ticker

6/recent/ticker-posts

TCRA YAENDESHA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imetoa  Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Kazi na Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta.

Akizungumza wakati wa semina hiyo iliyofanyika leo Jumatano Juni 21,2023 katika Ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga, Mhandisi Mihayo amesema lengo kuu la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha waandishi wa habari wanatambua majukumu ya TCRA na kuzijua sheria na taratibu ili wafanye kazi vizuri pamoja kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Mhandisi Mihayo ametumia fursa hiyo kuwashauri na kuwatahadharisha wadau wa mawasiliano wanaotaka kuanzisha vyombo vya habari mfano Redio kuepuka kutumia  watu ambao sio sahihi 'Vishoka' ambao wanawatumia ili kupata leseni kwani wengi wao ni matapeli  badala yake wawasiliane na TCRA ili kusaidia kupata huduma.

"Ni vyema wadau wa Habari wenye nia ya kuanzisha vyombo vya habari mfano vituo vya Radio nchini kuacha kutumia vishoka. Mkitaka kuanzisha radio ndugu zangu fuateni taratibu ambazo TCRA tunaelekeza na muachane na wale Vishoka ambao mwisho wa siku wataishiA kuwaibia tu pesa zenu na mnajikuta mnashindwa kufikia malengo yenu”, amesema Mhandisi Mihayo.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akitoa mada wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta

Mwezeshaji Edwin Soko akitoa mada kuhusu sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta

Viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa wakipiga picha na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga

Post a Comment

0 Comments