Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WANUFAIKA NA MRADI WA FORVAC, WAACHIWA VITENDEA KAZI KUJIENDELEZA.

Wajumbe wa kikao wakifuatilia kinachowasilishwa
Mratibu wa Mradi wa FORVAC, James Nshale.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akiongea na wqjumbe wa kikao.

*******************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


WANANCHI wanaoishi maeneo yenye mradi wa kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu wametakiwa kulinda na kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na vitendeakazi vya mradi huo vilivyoachwa baada ya muda wa mradi kumalizika.


Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ametoa wito huo jana kwenye kikao cha makabidhiano ya shuhuli zilizokuwa zinatekelezwa na Programu ya kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu (FORVAC) kwa Wilaya za Handeni na Kilindi kilichofanyika jijini Tanga.


Amesema mradi huo uliotekelezwa katika kipindi cha miaka minne umeleta ufanisi mkubwa kwa Wilaya husika hivyo inawapasa wananchi walioko maeneo hayo kutunza vifaa vilitumika kuutekelezea ili viweze kuendelea kufanyia kazi nyingine zitakazotokea.


"Wakurugenzi wote na wataalamu wa misitu ni vema mkaenda kuvisimamia vile vitendeakazi ili viendelee kuwepo, haitakuwa vizuri tena mwisho wa siku mnarudi kwa walioacha mradi mnatoa changamoto zenu, vile vifaa visije vikageuka vya kuharibu misitu badala ya kutekelezea mradi" amesema.


"Maofisa maliasili, kupitia elimu mliyoipata saa muende mkawajengee uwezo wananchi wenu ili wapate hizi taaluma wabaki nazo kuliko kuwaacha bila kupata tija kwa mradi huuunia sasa inakabiliwa na mabadiliko ya tabianchi, katoeni elimu wananchi watched kukata miti ovyo, badala yake wayatunze mazingira" amesisitiza.


Aidha Mgandilwa ameupongeza Ubalozi wa Finland kwa kuleta mradi nchini kwani umetekelezwa ipasavyo na kuleta maendeleo kwa vijana wengi ambao wamejiajiri kupitia mradi huo, huku wakijiunga kwenye vikundi na kupatiwa mikopo katika halmashauri zao


"Niupongeze sana Ubalozi wa Finland kwa kutuletea mradi huu nchini kwetu, umetekelezwa kwa tija na umetuletea faida, niombe kama kutakuwa na miradi mingine mtuletee Tanga kwa maana zile Wilaya zenye maeneo ambayo yanafaa kufanya mradi nazo zipate".


Naye Mratibu wa Programu ya kuongeza thamani mazao ya misitu Kitaifa James Nshale, amewataka vijana mkoani Tanga kujiunga kwenye vikundi na kujikita kwenye shuhuli za kujiajiri ili kunufaika na fursa zinazotolewa na serikali kwa kupatiwa mikopo ya halmashauri.


Nshale, amesema mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka minne kwani maendeleo yameonekana na sasa vijana na wanawake katika wilaya husika wanaendelea na shuhuli za kujiajiri huku akiishukuru serikali kwa kuwapa msukumo kwa kuwapa kipaumbele katika kuwapa mikopo.


"Vijana wa Wilaya za Handeni na Kilindi ambao wamepata bahati ya kufikiwa na mradi huu, wamefanikiwa kujiunga kwenye vikundi na wamepatiwa mikopo ya halmashauri zao, hivyo nitoe wito kwa vijana waweze kujifunza na kujiunga kwenye vikundi nao wapatiwe mikopo" amesema.


"Pia tunaishukuru sana serikali kwa kutoa ushirikiano wa kuwapatia mikopo vijana hawa ambao sasa wamejiajiri kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vyungu, mizinga ya nyuki na majiko ya kupikia" amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments