Ticker

6/recent/ticker-posts

WITO KWA WATALAAM KUTAFUTA TAKWIMU SAHIHI ZA UGONJWA WA BRUCELLA

Kaimu Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete akifungua warsha ya siku moja ya brucella ya wataalamu kutoka nchi za Tanzania na Rwanda tarehe 5 Juni, 2023 jijini Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji kitengo Cha Afya Idara ya Menejimenti ya ofisa ya Waziri Mkuu Dkt. Salum Manyata akiisistiza jambo wakati wa warsha iliyowakutanisha wataam kutoka Rwanda na Tanzania kuhusu ugonjwa wa Brucella iliyofanyika tarehe 5 Juni, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha.

Mratibu wa mradi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela Profesa Joram Buza akielezea hatua muhimu walizofikia ikiwemo kukusanya sampuli kutoka wilaya za Kwimba mkoani Mwanza na wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kwenye ranchi ya Kitengule.

Kaimu Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete ametoa wito kwa wataalamu kuwa na takwimu sahihi za chanzo cha ugonjwa wa brucella kwa binadamu na wanyama ili kuweza kuudhibiti.

Profesa Mshandete ameyasema hayo leo Juni 5, 2023 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa mwaka wa mradi wa brucella nchini Tanzania na Rwanda.

" wito wangu kwa wataalamu ni kuweka kipaumbele kwenye takwimu hizo zitakazowezesha kupata suluhisho la ugonjwa huo kama ilivyo kwa magonjwa mengine yanayopewa kipaumbele" amesema Profesa Mshandete


Aliongeza kwa kusema kuwa, takwimu sahihi zitasaidia serikali za Tanzania na Rwanda kupata njia za kuudhibiti ugonjwa wa brusella.

Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Afya, Idara ya Menejimenti ya Maafisa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Salum Manyata amesema uwepo wa takwimu sahihi utawezesha Nchi ya Tanzania yenye mifugo zaidi ya milioni 32 na binadamu millioni 60 kupanga na kuratibu njia sahihi na endelevu za kudhibiti ugonjwa wa brusella.

Aidha ameiasa jamii kufika kwa wataalamu wa afya pindi wanapopata homa mfululuzo kwani ni moja ya dalili za ugonjwa wa brucella na kuwashauri kuacha kunywa maziwa yasiyochemshwa na kuwa makini wakati wa kusaidia wanyama wanapozaa.

Naye Mratibu wa Mradi katika Taasisi hiyo Profesa Joram Buza amesema mpaka sasa wameshakusanya sampuli kutoka wilaya za Kwimba mkoani Mwanza na wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kwenye ranchi ya Kitengule.

Profesa Joram Buza amebainisha madhara ya ugonjwa wa brusella kwa wanyama ikiwemo kuharibika kwa mimba.

Amesema baada ya tafiti zote na kukusanya taarifa za ugonjwa wa brusella watakabidhi takwimu hizo serikalini ili ziweze kufanyiwa kazi na kudhibiti ugonjwa huo kwa binadamu na wanyama.

Post a Comment

0 Comments