Ticker

6/recent/ticker-posts

AS FAR RABAT YAMTANGAZA NABI KOCHA WAO MPYA

Mabingwa wa ligi kuu ya Morocco, AS FAR Rabat imemtangaza aliyekuwa kocha wa Yanga SC, Nasreddine Nabi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi.

Nabi ameondoka Yanga baada ya kufanikiwa kuiwezesha timu hiyo kutinga fainali kwa mara ya kwanza Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo aliondoka kutokana na mkataba wake kufikia tamati.

Kocha huyo ilitegemewa atakuwa kocha wa Kaizer Chief lakini matumaini iligonga mbwa baada ya miamba hiyo ya Madiba kumtangaza kocha mwingine na inasemekana walishindwana na Nabi kwenye upande wa masilahi.

Post a Comment

0 Comments