Ticker

6/recent/ticker-posts

BWAWA LA MAJI KIDUNDA KUKUZA UCHUMI WA NCHI


Utekelezaji wa mradi wa Bwawa la Kidunda umetajwa kama moja ya miradi wezeshi katika kukuza uchumi wa Taifa.
Fursa za kiuchumi zinazotajwa ni pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika, utalii, uvuvi, kilimo cha umwagiliaji na shughuli za kibiashara hususani katika Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam ambayo inaguswa na mradi huu wa kimkakati.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), Ndugu Laston Msongole anabanisha hayo wakati wa ziara ya Bodi hiyo katika eneo la ujenzi wa Bwawa la Kidunda, mradi unaotekelezwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia DAWASA kwa gharama ya Shilingi Bilioni 335.

“Tumekuja kushuhudia utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji unaogharamiwa na Serikali yetu na sisi (DAWASA) kama wasimamizi wa mradi tumekuja kujiridhisha utekelezaji ili kuhakikisha maslahi mapana ya Taifa yanazingatiwa.

Bw. Msongole amesisitiza kuwa DAWASA itasimamia kikamilifu mradi ili kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa pamoja na kukamilika kwa ubora, ndani ya muda uliowekwa ili hatimaye kuleta nafuu ya upatikanaji wa huduma ya maji majira yote ya mwaka.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Bw. Kiula Kingu amesema ziara ya Bodi ya Wakurugenzi katika mradi wa Bwawa la Kidunda inalenga kujionea kasi na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kwakuwa ndio wasimamizi wa Mamlaka kwa niaba ya Serikali.

Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilion 335 na unaotajwa kuwa muarobaini wa changamoto ya maji kwa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani. Mradi unatekelezwa na Mkandarasi Synohydro Ltd ya China kwa muda wa miezi 36 kuanzia Juni, 2023.



Post a Comment

0 Comments