Ticker

6/recent/ticker-posts

CCM TANGA YAOMBA USHIRIKIANO, WASIOKUWA NA SERA WAKACHEZEE MBALI.Na Hamida Kamchalla, TANGA.

CHAMA cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Tanga kimewasihi wadau wa maendeleo na wananchi kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na uhalifu hususani dawa za kulevya na mimba na ndoa za utotoni.

Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Tanga Rajabu Abdalla ameyasema hayo alipokuwa akizindua shina la wakereketwa Ccm mtaa wa Vatican City, kata ya Msambweni jijini Tanga ambapo pia amewataka wananchi kuacha kusikiliza maneno ya upotoshaji kuhusu maendeleo yanayofanywa na serikali.


"Shina hili liendelee kutumika katika maswala mbalimbali ya kimaendeleo na kupibga vitendo vya uhalifu ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya lakini mimba na ndoa za utotoni pamoja vitendo vingine viovu" amesema.


Amesema wapo baadhi ya viongozi wa vyama pinzani wanaopotosha kuhusu suala la bandari huku akieleza kwamba ni kutokana na kukosa sera hivyo amewasihi wananchi kuendelea kushikilia misimamo yao na kutokubali kulaghaiwa na kupotoshwa.


"Rais wetu na mradi wa bandari, aupeleke Bungeni kujadiliwa kisha uletwe kwa wananchi waujadili, halafu ndani yake kuwe na kitu kibaya, hii haiingii akilini, wenzetu wamekosa ajenda kwahiyo hii ndio wameona ni ajenda yao,


"Niwqambieni tu, Ccm Mkoa wa Tanga hii siyo ajenda, kama wameamua kutafuta kura kwa njia hii kwa Tanga hapana, tuko imara na tumejipanga kuliko wao wanavyofikiria, wakatafute mahala penngine pa kuchezea na kudanganya siyo hapa, wananchi hawataki kudanganywa bali wapo tayari kumuunga mkono Mh. Rais Samia Suluhu Hassan" amesema.


Mbali na hayo Mwenyekiti alikabidhi kiasi cha shilingi m 1.2 kwa ajili ya mtaji wa shina hilo lakini pia aliahidi kuwawekea kiasi cha sh m 1 kwa ajili ya kuunga mkono maendeleo ya tawi na wanachama wake.

Post a Comment

0 Comments