Ticker

6/recent/ticker-posts

CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA CHASHIRIKI MAONESHO YA 18 ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


WASHIRIKI kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika (EASTC) wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la Chuo hicho wakati wa Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Na.Alex Sonna-DAR ES SALAAM

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimeshiriki Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yameanza Julai 17, 2023 na yatahitimishwa Julai 22, 2023

Akizungumza kwenye banda la taasisi hiyo Mkuu Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika (EASTC), Dkt. Tumaini Katunzi amewataka wananchi na wanafunzi kutembelea banda la chuo hicho ili waweze kupata maelezo juu huduma za elimu na ushauri kuhusu maswala ya kitaaluma ikiwemo udahili wa wananfunzi waliomaliza kidato cha nne na kidato cha sita.

”Tunawakaribisha wananchi pamoja na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na cha sita kupata elimu pamoja na kufanya udahili ambao tunaufanya bure kabisa bila malipo yoyote”amesema Dkt. Katunzi.

Pia, Dkt. Katunzi amewaalika wanafunzi na wananchi wote kuomba nafasi za masomo ya takwimu na tehama kwa ngazi ya cheti na diploma pamoja na Shahada ya Uzamili katika Takwimu yatakayoanza rasmi mwaka huu katika Kampasi ya Dodoma kwenye majengo ya Chuo Kikuu Huria mtaa wa Uzunguni.

Naye ndugu Eusebius Mwisongo, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo hicho, anakaribisha wananchi kutembelea banda la Chuo hicho kwani timu nzima ya masoko ipo tayari kuwahudumia na kutoa elimu kwa undani zaidi kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Aidha amwaomba wananchi kuendelea kutembelea tovuti ya chuo www.eastc.ac tz ambapo watapata taarifa zaidi na mawasiliano ya watoa huduma kwa ufafanuzi zaidi.

Post a Comment

0 Comments