Ticker

6/recent/ticker-posts

DC TEMEKE AMWAKILISHA RC DAR KUMPOKEA WAZIRI MKUU BURUNDI

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Temeke Dar es Salaam Mobhare Matinyi amemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Albert Chalamila kumpokea Waziri Mkuu wa Burundi, Gervais Ndirakobuca.

Waziri Mkuu Ndirabobuca amewasili jana Julai 24, 2023 saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa nchi za Afrika wanakusanyika jijini Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano wa Afrika wa Rasilimali Watu unaofanyika tarehe 25-26 Julai, 2023. Mwenyeji wa mkutano huo ni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

0 Comments