Ticker

6/recent/ticker-posts

EWURA YAWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU UPATIKANAJI WA MAFUTA


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa uhakika wa mafuta nchini baada ya kutembelea maghala ya kuhifadhia mafuta jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo iliyoongozwa na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, na kujumuisha watendaji wa EWURA, PBPA, TAPSOA, TPA na Wizara ya Nishati, ilifanywa katika kampuni za mafuta za TIPPER,LAKE OIL,MOUNT MERU,MOIL,CAMEL OIL, TOTAL ENERGIES na PUMA.

Mh. Makamba na ujumbe wake pia walitembelea eneo la kupokelea mafuta katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujiridhisha kuhusu uingiaji na upakuaji wa bidhaa za petroli.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA , Dkt James Andilile, alisema ziara hiyo ni utekelezaji wa wajibu wa EWURA kusimamia na kufuatilia mwenendo wa upatikanaji wa mafuta nchini na ametumia fursa hiyo kuwasihi watumiaji wa mafuta kutokuwa na hofu kwani hakuna uhaba wa mafuta.

Post a Comment

0 Comments