Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA VIONGOZI MBALIMBALI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU RASILIMALI WATU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mama Graca Machel, mke wa zamani wa aliyekuwa Rais wa Msumbiji, Samora Machel ambaye pia ni Mwanasiasa na Mtetetzi wa Haki za Binadamu kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova mara baada ya mazungumzo Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Uganda Mhe. Jessica Rose Epel Alupo kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Mhe. Hussein Abdelbagi Akol Agany kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu wa Somalia Mhe. Hamza Abdi Barre kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto, Rais wa Malawi Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera, Rais wa Madagascar Mhe. Andry Rajoelina, Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova pamoja na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Bio wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri kutoka Ofisi ya Rais ya Namibia Mhe. Christine Hoebes mara baada ya mazungumzo yao Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.

Post a Comment

0 Comments