Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MASUALA YA JINSIA


Na WMJJWM, DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.John Jingu amekutana na kufanya Mazungumzo na Mwakilishi wa shirika la linalojishughulisha na masuala ya Jinsia la NIRAS Tanzania Dkt. Suma Kaare pamoja na Mwakilishi wa Umoja wa ulaya Guidet Chiara leo Julai 03, 2023 Jijini Dodoma.

Kikao hicho kilikua na lengo la kuwatambulisha wataalam wasaidizi sita wa shirika hilo watakaofanya kazi kwa kushirikiana na Serikali kutekeleza Mradi wa GENDER TRANSFORMATIVE ACTION, BREAKING THE GLASS CEILING IN TANZANIA, unaofadhiliwa na umoja wa Ulaya ili kutekeleza afua za kupinga ukatili na kuwezesha usawa Kijinsia nchini.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Sifuni Msangi.


Post a Comment

0 Comments