NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
TAASISI ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) imekuwa inatoa huduma kulingana na mahitaji ya mteja na wao wanabuni ii kukidhi mahitaji, hivyo imeshiriki Maonesho ya 47 ya biashara Dar es salaam(DITF) maarufu kama sabasaba ambapo imekuja na mashine za kuchakata zabibu (Grape Crusher Destemmer).
Akizungumza katika Maonesho hayo, Afisa Masoko (TEMDO), Dkt.Sigisbert Mmasi amesema wameamua kuwasogezea wajasiriamali mashine za kuchakata zabibu kwa ajili ya viwanda vya "wine" kwani mashine hiyo itamuwezesha kuchakata zabibu takribani kilo 700 kwa saa moja.
Aidha amesema wwamekuja na mashine mbalimbali kwa upande wa kilimo ambapo wanamashine ya kukamua mafuta ya alizeti au ufuta zinaziweza kukamua kilo 3000 kwa siku pamoja na mashine za kuchakata mihogo Tani 12 kwa siku moja.
"TEMDO imelenga katika ukuzaji wa thamani wa mazao ya kilimo hivyo imejikita katika uzalishaji mkubwa,kwa wakulima wanao weza kununua mashine kwa vikundi wataweza kumiliki mashine kwa ajili ya uzalishaji,Ila hata mtu binafsi naye anaweza kununua". Amesema
Amesema kwa upande wa sekta ya afya amesema wamepata ithibati ya vifaa tiba vya aina kumi na saba (17), wamekwisha andaa vifaa tiba vya aina Saba ambavyo viko tayari,kitanda cha mgonjwa, kiteketezi taka za taka za hospitali ambacho hakitaleta madhara ya kikemikali kwa binadamu.
Hata hivyo amesema kuwa wanatoa Mafunzo ya uhandisi viwandani kwa wahandisi na mafundi kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa uzalishaji ambapo ofisi zao zipo mkoani Arusha .
Afisa Masoko (TEMDO), Dkt.Sigisbert Mmasi akiwaelezea baadhi ya wananchi namna mashine ya kuchakata zabibu (Grape Crusher Destemmer)inavyofanya kazi mara baada ya kutembelea banda la TEMDO katika Maonesho ya 47 ya biashara Dar es salaam(DITF) maarufu kama sabasaba Julai 6,2023 Jijini Dar es Salaam.
0 Comments