Ticker

6/recent/ticker-posts

TET YASHIRIKI MAONESHO YA 47 YA BIASHARA KIMATAIFA SABASABA

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) inashiriki Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) ambapo wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo uuzaji wa vitabu vya kiada kwa shule za msingi na Sekondari.
Pamoja na hayo TET kwenye Maonesho hayo inatoa elimu juu ya maktaba mtandao ambapo Mwalimu na Mwanafunzi wanaweza kujisomea na kupata maarifa zaidi kupitia maktaba hiyo.

Pia TET imeandaa meza maalum ya hadithi za watoto zenye kuelimisha, kuburudisha na kuwaongezea maarifa watoto.
Wanapatikana katika Jengo la Jakaya Kikwete chumba na 1 mpaka 3.

Post a Comment

0 Comments