Ticker

6/recent/ticker-posts

UDSM YAWAKUTANISHA WANAFUNZI WA SHAHADA YA KWANZA YA MADINI NA JIOSAYANSI NA WAAJIRI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam kupitia Idara ya Shule Kuu ya Madini na Jiolojia imewakutanisha wanafunzi wanaoendelea na mafunzo na wanaohitimu shahada ya kwanza ya madini na Jiosayansi chuoni hapo kwa lengo la kuwakutanisha na waajiri na kuwaonyesha fursa katika idara hiyo.

Akizungumza wakati akifungua hafla hiyo kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam-Utafiti, Prof.Nelson Boniface amesema lengo la kuwakutanisha wanafunzi hao na watalaamu mbalimbali ni kuhusisha wanachosoma na mazingira ndani ya jamii.

Amesema ni muhimu wanafunzi hao kutumia kila fursa wanayoipata kukuza taalamu zao kwa kujiajiri au kuajiriwa hivyo kupitia hafla hiyo ambayo watu mbalimbali wamealikwa ambapo watatoa mada kwaajili ya kuwaandaa vijana hao kwenye masuala ya fursa kupitia idara hiyo.

Nae Amidi wa Shule ya Madini na Jiolojia chuoni hapo Dk Elisante Mshiru amesema idara hiyo ina mkakati wa muda mrefu na mfupi wa kuongeza wataalamu wa madini.

"Sasa hivi upo mchakato unaoendelea wa kuboresha mitaala na pia kuna mapinduzi ya nishati yanaendelea, tutazingatia namna gani mitaala yetu inajikita huko". Amesema

Kwa upande wa washiriki wa hafla hiyo wamesema kuwa hafla hiyo ni muhimu kuwatambulisha kwenye soko la ajira na kubaini fursa zilizopo katika sekta hiyo.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam-Utafiti, Prof.Nelson Boniface akizungumza katika Hafla ya kuwaaga Wanafunzi wa Shule Kuu ya Madini na Jiosayansi ambapo Chuo kimealika watu mbalimbali ambao wametoa Mada kwaajili ya kuwaandaa vijana kwenye masuala ya fursa zinazopatikana kwa vitu ambavyo wamesome. Tukio hilo limefanyika leo Julai 15,2023 UDSM Jijini Dar es SalaamAmidi Shule Kuu ya Madini na Jeosayansi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Elisante Mshiru akizungumza katika Hafla ya kuwaaga Wanafunzi wa Shule Kuu ya Madini na Jiosayansi ambapo Chuo kimealika watu mbalimbali ambao wametoa Mada kwaajili ya kuwaandaa vijana kwenye masuala ya fursa zinazopatikana kwa vitu ambavyo wamesome. Tukio hilo limefanyika leo Julai 15,2023 UDSM Jijini Dar es Salaam


Post a Comment

0 Comments