Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKENDA ASEMA VITUO VYA STEM PARKS KUJENGWA NCHI NZIMA, JIJI LA DODOMA KUTOA ENEO

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia Adolf Mkenda amesisitiza tekinilojia kutumika zaidi ili nchi kuendana na kasi ya ulimwengu wa sayansi ambapo kuna mpango wa kujengwa vituo vingi vya masomo hayo nchi nzima.

Ameyasema leo alipotembelea kituo cha saysnsi cha STEM Park kilichopo jijini Tanga wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo kwa lengo la kujua maendeleo ya sayansi na tekinolojia.


"Nimetembelea kituo hiki cha sayansi ili kuona maendeleo ya elimu ya sayansi na tekinolojia, hapa nimeona vitu vizuri wanavyofundisha kupitia tekinolojia, tunakoelekea hakutakuwa na mwalimu ataingia darasani na kuandika kwenye ubao bali watakuwa wakitumia tekinolojia kwa kuwafikirisha wanafunzi wajifunze mpaka waelewe wenyewe" amesisitiza Waziri.


"Hii Park ni kitu kimoja cha umuhimu sana ambacho kitakwenda kuchochea utundu na uelewa wa vijana, hapa nitoe pongezi kwa halmashauri ya jiji la Tanga kwa kutoa eneo hili ambalo wenzetu wamejenga Park hii na kuwawezesha vijana wetu" amesema.


Mbali na hayo amesema kwamba Wizara ina mpango wa kujenga vyuo vingi nchini ili watoto wengi wapate kujifunza na kwa kuanzia litatengwa eneo kubwa jijini Dodoma ma kujenga kituo kikubwa ambacho kitakuwa cha mfano na kila Mkoa utajengwa.



Naye Mkurugenzi wa kituo cha saysnsi cha STEM Park, chini ya Project Inspire, Dkt. Lwidiko Mhamilawa amesema wanafundisha wanafunzi kutokana na udadisi wao wa kiakili ya sayansi na kuwawezesha mpaka kufikia kuwa wana sayansi halisi.


"Hii ni kufundisha kupitia mbinu mbalimbali ikiwemo miradi, lakini pia kuandaa mazingira mazuri ya kujifunzia kama vile kujenga STEM Parks, ambazo kwasasa zipo hapa Tanga na Dar es salaam, pamoja na kuwapatia fursa na kuwashikilia tangu wakiwa wadogo na kuhakikisha wanajifunza na kupata hamasa ya kuipenda sayansi" amesema.


"Kwa nchi zilizoendelea takribani asilimia 60 mpaka 70 ya mapato yao yanatokana na tekinolojia, sayansi, uhandisi na mahesabu, na ili Tanzania tuweze kufika huko tunahitaji wanataaluma wengi, kwahiyo ndiyo maana tunafanya hivi kwa miaka 8 sasa" amesisitiza Mkurugenzi.


Vilevile Dkt. Mhamilawa amesema tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2021 wamekuwa wakipata wanafunzi tofauti tofauti kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Tanga na mpaka kufikia sasa tayari wameshatoa mafunzo kwa watu wapatao 30 elfu kituoni hapo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Tekinolojia (COSTECH) Amos Nungu amesema kama ilivyokuwa kwa COSTECH, STEM pia inasaidia kuhamasisha na kujifunza maswala ya sayansi, tekinolojia na hesabu kwa ufanisi zaidi, kujenga uelewa kwa wanafunzi.


"Mradi kama huu ulianzia pale COSTECH, tuna ukumbi wa ubunifu na wanafundisha kwa vitendo, hapa tulipofikia sasa tunamwambia Muheshimiwa Waziri kwamba hamasa ni kubwa na vituo hivi viendelee kujengwa ili uhamasishaji wa masomo ya sayansi na tekinolojia ikue zaidi" amefafanua.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia Adolf Mkenda akielekeza jambo alipotembelea katika kituo cha saysnsi cha STEM Park.

Mkurugenzi wa kituo cha saysnsi cha STEM Park Dkt. Lwidiko Mhamilawa akifanya haribio la kutengeneza nishati ya gesi mbele ya Waziri Mkenda.

Waziri Mkenda akiongozana na time yake wakiwa wanasikiliza maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa kituo hicho.

Waziri Mkenda akieleza jambo wakati akiendelea kufanya ukaguzi kituoni hapo.

Post a Comment

0 Comments