Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDALICHAKO ASISITIZA WAFANYAKAZI WA HOTELI ZA KITALII UTOAJI WA HUDUMA BORA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako ,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 637,yaliyomalizika leo Julai 29, 2023 jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 637,yaliyomalizika leo Julai 29, 2023 jijini Arusha.


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzanne Ndomba,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 637, leo Julai 29, 2023 jijini Arusha.


Mkurugenzi wa Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 637, leo Julai 29, 2023 jijini Arusha.


Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani),akizungumza wakati akifunga mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 637,yaliyomalizika leo Julai 29, 2023 jijini Arusha.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufunga mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 637,yaliyomalizika leo Julai 29, 2023 jijini Arusha.Na: Mwandishi Wetu - Arusha

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako amewataka wafanyakazi wa hoteli za kitalii kutoa huduma bora kwa wageni ili kutimiza azma ya Serikali kufikia lengo la watalii milioni tano kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.

Prof. Ndalichako amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 637, leo Julai 29, 2023 jijini Arusha ambapo amebainisha kuwa sekta ya utalii inakua kwa kasi na sasa Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa Afrika.

Amesema uamuzi wa ofisi hiyo kutoa mafunzo hayo umetokana na ripoti ya utafiti mdogo uliofanywa kuonyesha sekta hiyo inakabiliwa na huduma zisizoridhisha.

"Baada ya kufanywa tathimini, Ofisi yangu pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii tulibaini hoteli 35 zinazotoa huduma mbalimbali kwa wageni hazitoi huduma zenye viwango, ikiwemo huduma zisizoridhisha, lugha mbaya na usomaji wa simu janja bila kujali wateja," amesema.

Prof. Ndalichako amesema kutokana na changamoto hiyo wizara hiyo imetoa mbinu mbalimbali za mafunzo kwa ajili ya kuongeza ujuzi zaidi na kwamba ujuzi huo utaleta tija katika sekta ya hoteli ikiwemo kuongeza vipato kwa wafanyakazi ambao wanatoa huduma nzuri na kwa wakati.

Amesema suala la ujuzi ni nyenzo muhimu ya kuvutia wageni na kuendelea kuchochea sekta hiyo.

Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu, amesema mafunzo yanatolewa kupitia programu ya Taifa ya kukuza ujuzi inayolenga kuwawezesha wasio na ajira kupata mafunzo ya uanagenzi na uzoefu kazini ili kuongeza tija kwa nguvukazi katika soko la ajira.

Kwa upande mwengine, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Suzanne Ndomba amesema ni muhimu vijana wapate mafunzo wakiwa kazini ili kufikia malengo waliyojiwekea katika kuondokana na changamoto za ujuzi, pia kutoa huduma bora huku Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Henry Mkunda amesisitiza mafunzo hayo yawe chachu ya kuleta maendeleo hususan katika sekta ya hoteli na utalii.

Post a Comment

0 Comments