Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA BALOZI MSTAAFU WA MAREKANI NCHINI TANZANIA MHE. MARK GREEN JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Wilson Centre na Balozi Mstaafu wa Marekani nchini Mhe. Mark Green aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Wilson Centre na Balozi Mstaafu wa Marekani nchini Mhe. Mark Green pamoja na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Mama Salma Kikwete, Mke waRais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation Bi. Vanessa Anyoti, wakiwa na mama Suzan Green, mke wa Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Wilson Centre na Balozi Mstaafu wa Marekani nchini Mhe. Mark Green baada ya kutembelea hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam leo.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Wilson Centre na Balozi Mstaafu wa Marekani nchini Mhe. Mark Green aliemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Wilson Centre na Balozi Mstaafu wa Marekani nchini Mhe. Mark Green pamoja na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Katibu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) na kulia kabisa ni Dkt. Catherine Sanga Meneja wa Miradi wa JMKF na kushoto kabisa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa JMKF Bi. Vanessa Anyoti.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi ya picha waliyopigwa January 13, 2009 (miaka 12) iliyopita Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Wilson Centre na Balozi Mstaafu wa Marekani nchini Mhe. Mark Green ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwa balozi ni Mama Suzan Green, mke wa balozi Green.

Picha na Issa MichuziPost a Comment

0 Comments