Ticker

6/recent/ticker-posts

MAENDELEO BANK YATANGAZA GAWIO KWA WANAHISA LA SH.708 MILIONI KWA MWAKA WA FEDHA WA 2022

MAENDELEO BANK imetangaza gawio kwa wanahisa la shilingi Milioni 708 kwa mwaka wa fedha wa 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 136 ikilinganishwa na gawio la shilingi 11 kwa hisa la mwaka 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkuu Idara ya Usimamizi wa Athari na Taratibu za Benki, Bw.Peter Tarimo amesema katika mkutano uliofanyika hivi karibuni walipitisha kwa kauli moja mapendekezo ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusu malipo ya gawio la Shilingi 26 kwa kila hisa ambayo yanaleta jumla ya gawio la Shilingi milioni 708.

Amesema gawio kwa Wanahisa litalipwa tarehe 6 Octoba 2023 kwa wanahisa wote watakaokuwa kwenye regista ya Wanahisa kwa tarehe 31 Augusti 2023.

“Gawio hili, ni mgao wetu wa nne na wa pili kwa pesa taslimu tangu kuanzishwa kwa benki mwaka 2013 , hii inaonyesha dhamira ya benki kuwatuza wenyehisa kwa umiliki wao”. Amesema Bw.Tarimo.

Aidha amesema Benki ilipata faida kabla ya kodi ya shilingi milioni 1,984 kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2022 (2021: TZS milioni 706 ) na mapato baada ya kodi yalikuwa shilingi milioni 1,416 ikiwa ni ukuaji wa 141% ikilinganishwa na shilingi milioni TZS 587 mwaka 2021.

Amesema katika mwaka huo juhudi kubwa zilifanywa ambapo faida ya benki iliongezeka kwa sababu ya kutafuta njia mpya za biashara na kuendelea kutoa huduma za kiushindani.

Pamoja na hayo amesema kuwa juhudi za uwekezaji zilizofanywa katika mwaka huo zilisababisha ongezeko la 31% katika viwango vya riba. Mapato halisi ya riba yalikua mwaka hadi mwaka hadi kufikia shilingi milioni 9,911 kutoka shilingi milioni 7,538 mwaka 2021.

Ameeleza kuwa Ongezeko la mapato ya riba halisi ni matokeo ya ongezeko la mikopo la shilingi milioni 2,942 kutoka baki ya mikopo ya shilingi 57,716 mwaka 2021 hadi milioni TZS 60,658 mwaka 2022. Riba ya uwekezaji katika dhamana iliongezeka kwa shilingi 1,667 kutoka shilingi 2,089 mwaka 2021 hadi shilingi milioni 3,756 mwaka 2022



Mkuu Idara ya Usimamizi wa Athari na Taratibu za Benki, Bw.Peter Tarimo akizungumza na waandishi wa habari leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wakitangaza gawio kwa wanahisa.

Post a Comment

0 Comments