Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE MTATURU ALIGUSA JESHI LA AKIBA


MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ametimiza ahadi yake aliyoitoa siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwa kukabidhi seti mbili za jezi za michezo kwa vijana walio kambini kwenye mafunzo ya Jeshi yanayofanyika kiwilaya katika Kata ya Unyahati.

Akikabidhi jezi hizo Agosti 2,2023,Katibu wa mbunge Ally Rehani amesema Mtaturu ametoa vifaa hivyo kama sehemu ya kuhimiza michezo ili kuimarisha afya za wananchi.

“Kama tunakumbuka Mbunge wetu siku ya Mashujaa alikabidhi mipira miwili na kutoa ahadi ya kuleta seti za michezo ambazo leo amekuja kutimiza ahadi yake,”.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Thomas Apson,Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Rashid M.Rashid amemshukuru mbunge kwa kutoa vifaa hivyo vitakavyokuwa na msaada mkubwa wakati wote wa mafunzo kwa vijana wa jeshi la akiba.

Vijana hao wapatao 138 wameanza mafunzo hayo mapema mwezi uliopita yatakayowachukua miezi mitatu.

Post a Comment

0 Comments