Ticker

6/recent/ticker-posts

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa aipongeza RUWASA Bukoba auzindua mradi wa maji rasmi.


Na Shemsa Mussa , Kagera.

Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ndg Abdalla Shaib Kaim ameridhia kukagua na kuuzindua mradi wa maji Kashenge - Ilogero uliyopo katika kata katoma ndani ya Halmashari ya Bukoba, na huku
akiwasisitiza wananchi kulinda na kuitunza miradi ambayo inajengwa ili kutimiza adhima na nia ya serikali.

"Tunajua serikali inawapenda sana wananchi wake na inahakikisha inatatua changamoto nyingi ikiwemo ya maji na kumtua mama ndoo kichwani na pia serikali yetu haipendi kuona wananchi wake wanateseka nitashangaa sana kuona mradi mzuri na mkubwa hivi unaharibiwa hivyo kila kinachofanywa na serikali kitunzeni jamani amesema Ndg Kaim".

Nae Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Evaristo Mgaya baada ya mwenge wa Uhuru kuzindua mradi huo mkubwa wa maji August 10 amesema mradi umegharimu zaidi ya shilingi milioni 768 pia mradi huo unatokea katika kata ya Karabagaine na kuleta maji Kata ya Katoma hivyo wananchi wa kata hizo amewanata kutunza na kuulinda mradi huo ili utumike kwa vizazi vya sasa na vijavyo na hasa kuhakikisha wanalinda na kutunza chanzo cha maji Kyeiringisa kwa kutofanya shughuli za kijamii katika chanzo hicho kwani kikikauka wataendelea kupata changamoto ya maji

" Ndugu zangu wananchi tanajua kuwa mradi wa maji ni chanzo na chanzo kikishakauka upatikanaji wa maji utakuwa mgumu na pia mradi hautokuwa na faida kwenu naomba sana tusifanye shughuli yoyote ya kibinadamu kama kuchoma Moto karibu na chanzo pia kulima sehemu ya chanzo , amesema Mhandisi Mgaya ".

Pia Mhandisi Mgaya ameongeza kuwa mradi huo wa maji ni mkombozi wa tatizo la upatikanaji wa maji ambalo limekuwa likiwakumba wananchi wa vijiji hivyo kwa muda mrefu hivyo ni matarajio ya serikali kuwa mradi huo utakuwa kichocheo cha maendeleo kwa wananchi na unatarajia kuwahudumia wananchi zaidi ya 7,000

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kata ya Katoma wamesema kuwa kuzinduliwa kwa mradi huo kutawasaidia kuepukana na changamoto waliyokuwa wanapata kwani iliwalazimu kuamka saa kumi za usiku kwenda kuchota maji kwenye vyanzo vya asili na maji hayo hayakuwa safi na salama hivyo wanaishukuru serikali kwa kuwakumbuka na kuwajengea mradi huo.

Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika halmashauri ya Bukoba vijijini na umetembelea,kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na utakabidhiwa August 11 katika Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera.

Post a Comment

0 Comments