Ticker

6/recent/ticker-posts

RC NA WANAOTAKA KUHARIBU AMANI, WALEMAVU WAOMBWA KUVUMILIA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akiongea kabla ya kufungua mafunzo.
Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tanga Tonny Mwanyota akitoa taarifa ya takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Baadhi ya wakufunzi wa mafunzo hayo wakifuatilia mafunzo.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga wakifuatilia mafunzo.

*******************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

SERIKALI Mkoani Tanga imeonya kwamba hatovumiliwa mtu au kikundi cha watu watakaoingia mkoani humo kujaribu kutaka kuvunja amani na utulivu kwa wananchi badala yake hatatoka salama.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, kwa viongozi, watendaji, wawakilishi wa vyama vya siasa na makundi maalumu wa Mkoa na halmashauri zake uliofanyika jijini Tanga.


"Yeyote atakayekuja na wazo la kutaka kuvunja amani yetu katika Mkoa huu, akilianzisha sisi tutalimaliza, hatutaki tabu tunataka amani yetu iendelee na anayetaka shida aishie kwenye mipaka asiingie katika Mkoa wetu " amesema.


Akizungumzia lengo la mafunzo hayo, Kindamba amesema ni kuwajengea uwezo wakufunzi kuchambua na kutumia matokeo ya sensa ili yawe mwanzo wa dira ya kuwaongoza katika utekelezaji wa majukumu na malengo yao ya kila siku.


"Mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kutafsiri, kwahiyo nawaomba sana wakati mafunzo yakiendelea kuwa watulivu, ili yaweze kwenda kuwa msaada kwenye ngazi ya chini" amefafanua.


Kindamba amebainisha kwamba kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 idadi ya watu Mkoa wa Tanga idadi imeongezeka lakini siyo kwa idadi kubwa ya watu tofauti na Mikoa mingine Kitaifa.


"Idadi yenu inaonesha kwamba, kiwango chenu cha kuongezeka kimetoka asilimia 2.2 mwaka 2012 na kufikia asilimia 2.5 2022, lakini pamoja na hayo, Mkoa wa Tanga inaonesha kwamba kasi yetu ya kukua iko chini sana ikilinganishwa na takwimu za sensa za Kitaifa ambazo sasa ipo asilimia 3.2" amesema.


Kufuatia hali hiyo, Kindamba amewataka viongozi wa halmashauri kuwa making zaidi katika kuhakikisha wanaweka mikakati madhubuti na endelevu itakayowahakikishia wananchi huduma bora na za kiuchumi ili kuimarisha ustawi wao na maendeleo ya Mkoa.


"Lakini pia ni muhimu kutambua kwamba Mkoa wetu unafunguka, hii maana yake uyanakuja mambo mengi, kwa mfano kuna mradi mkubwa wa bomba la mafuta nao utakuja na watu wake, lakini pia sisi tumeamua Tanga iwe kituo cha kuvutia watu waje, kwahiyo wanapokuja na wenyeji nao wapo" amesema.


Naye Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tanga Tonny Mwanyota amewaomba wadau wa sensa na wananchi kwa ujumla kuwa wavumilivu kwa baadhi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, kusubiria majibu ya matokeo kwa upande wa watu wenye hali ya ulemavu.


Mwanyota amesema matokeo ya sensa bado yanaendelea kutolewa kwa awamu hivyo kwa ugumu wa takwimu kwa wenye ulemavu hivyo nayo yapo miongoni mwa yale ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi.


Mwanyota amesema watu wengi wamekuwa wakiuliza sana kuhusiana na ripoti ya watu wenye ulemavu swali ambalo limekuwa likijirudia mara kwa mara lakini ametoa ufafanuzi juu ya jambo hilo na kusema, "ripoti hii moja kati ya zile zinazoandaliwa, hivyo tunaomba subira kutoka kwa wadau wote wa takwimu za watu wenye ulemavu".


"Kwa upande mmoja watu wanadhani tumemaliza zoezi hili la sensa, kukamilika kwa kuhesabu watu siyo mwisho, bado tuna kazi nzito inaendelea, tofauti na sensa zilizopota, mwaka huu kumekuwa na hamasa kubwa ya wadau kutaka matokeo wakidhani kama wanacheleweshwa" amefafanua.

Post a Comment

0 Comments