Ticker

6/recent/ticker-posts

TPA INASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA 95 YA KILIMO NA BIASHARA NCHINI ZAMBIA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inashiriki katika maonyesho ya 95 ya Kilimo na Biashara yanayofanyika Lusaka Nchini Zambia.

TPA inashiriki katika maonyesho hayo kama moja ya Kampeni za Kimasoko na Elimu kwa Umma na Wadau zenye lengo la kutangaza Huduma za TPA ili kuongeza idadi ya Wateja na kiwango cha Shehena katika Bandari za TPA

Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Luteni Jenerali Mathew Mkingule ametembelea Banda la TPA katika maonesho hayo.

Balozi Mkingule ameipongeza TPA kwa kudhamini na kushiriki katika maonyesho hayo na kutoa wito kwa Jumuia ya Wafanyabiashara Nchini Zambia na Nchi za SADC kuendelea kutumia Bandari za Tanzania na hasa Bandari kuu ya Dar es Salaam ambayo ina mchango mkubwa katika Sekta ya Uchukuzi kwa Tanzania na Nchi jirani ikiwemo Zambia.

Post a Comment

0 Comments