Ticker

6/recent/ticker-posts

VIJANA 260 KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA KILIMO CHA KISASA NCHINI ISRAEL

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imewezesha vijana 260 kwenda Israel kujifunza na kupata uzoefu katika fani ya kilimo na mifugo kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Akizungumza Agosti 26, 2023, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu katika hafla ya kuwaaga vijana hao jijini Dar es salaam, amesema mafunzo hayo yamegharamiwa kiasi cha Sh.milioni 256 na serikali kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na ofisi hiyo na kuwaasa vijana hao kutumia vizuri fursa hiyo.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Aijra na Ukuzaji Ujuzi wa Ofisi hiyo, Ally Msaki, amesema tangu mwaka 2019 serikali imepeleka vijana kutoka vyuo mbalimbali zaidi ya 700 nchini Israel kwenda kujifunza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Leonce Bilauli amesema vijana hao watapata mafunzo kwa kipindi cha miezi 11 na watapatiwa fedha za kujikimu.

Wakizungumza kwa niaba ya vijana wenzao, Halima Ramadhan na Gasper Gwamaka wameishukuru serikali kwa kuendelea kuwawezesha vijana kupitia programu mbalimbali na kuahidi kutumia mafunzo hayo kuleta mapinduzi ya kilimo cha kisasa nchini kwa kujiajiri na kuwaajiri wenzao.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga vijana wanaotarajia kwenda kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa nchini Israel iliyofanyika katika ukumbi wa Nkuruma jijini Dar es salaam tarehe 26 Agosti,2023.
Baadhi ya vijana wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ushirikiano wa Afrika Leonce Bilauli Mashariki akieleza jambo wakati wa hafla hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu akiwa kwenye picha ya pamoja na Vijana wanufaika wa mafunzo hayo pamoja na viongozi na watenda kutoka wizara na taasisi mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments