Ticker

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA WANANCHI LAKI 1 SAWA NA ASILIMIA 78 NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA WANATUMIA MAJI SAFI.





**************

Na Shemsa Mussa - Kagera.

Jumla ya wananchi laki 193052 sawa na asilimia 78 ya wakazi wanaoishi manispaa ya bukoba Mkoani Kagera wanatumia huduma ya maji safi. 
Amesema hayo Meneja Miundombinu kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (BUWASA)Eng Yazidi Bwikizo wakati akisoma lisala fupi mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa alipopita kukagua,kutembelea na kufanya zoezi la upandaji wa miti katika chanzo cha maji kagemu leo August 8.


Eng Bwikizo amesema kwa mujibu wa takwimu za sensa ya Mwaka 2022 Mji wa bukoba unao wananchi 144,938 na wananchi waliozungukwa na mtandao wa maji ni 133,342 na mpka sasa wananchi wanaotumia na kupata huduma ya maji safi ni 113, 053 sawa na asilimia 78 ya wakazi wote wanaoishi ndani ya Manispaa ya Bukoba .

Amesema chanzo cha maji kagemu kinahudumia ukanda wa juu na hutumika kwa dharura inapotokea matengenezo kwenye chanzo kikuu cha bunena na wakati wa kiangazi ili kuongeza upatikanaji wa maji ya kutosha pia amesema chanzo hicho kimeongeza uzalishaji kutoka Mita za ujazo elfu 2000 sawa na lita Milion 2 kwa siku hadi kufikia Mita za ujazo elfu 3000 sawa na lita Milion 3 kwa siku.

"Tunavyojua wakati wa kiangazi uhitaji wa maji unaongezeka na unakuwa mkubwa sana hivyo hukitumia chanzo hiki kwa ajili ya dharura hiyo na kwasasa tunayo maji ya kutosha yanayokidhi wananchi wa mji huu wa Bukoba tunajivunia kuongeza uzalishaji ,amesema Eng Bwikizo"

Pia amesema wameweza kudhibiti maji yaliyokuwa yakipotea wakati wa kiangazi na kujenga mifereji au njia ya kupitisha maji pindi yapojaa ili kuimalisha kitekeo pamoja na kutengeneza ubora mzuri wa maji kwa kuondoa tope (matope)lililokuwa likiingia kwenye kitekeo pia amesema mpaka sasa chanzo hicho kinahudumia kata za Kitendaguro,Kibeta,Ijuganyondo,Rwamishenye Inshambya pamoja na baadhi ya maeneo ya kata ya Hamgembe.

Naye kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg Abdalla Shaib Kaim ambaye amefika na kumulika chanzo hicho cha maji amesema kuwa ameridhishwa na mazingira yalivyopandwa miti , usafi pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara katika kituo hicho ikiwa ni ishara ya kukijari chanzo hicho na kuwajari wananchi pamoja na kutambua umuhimu wa maji amesema ameridhia kukikagua na kushiriki upandaji wa miti ili kuongeza nuru ya kuwa bora zaidi.

Ikumbukwe kuwa Mwenye wa Uhuru uliingia ndani ya Mkoa wa Kagera August 8 2023 na utaweza kukagua, kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali katika Halmashauri zote 8 za Mkoa kagera na utakabidhiwa August 16 2023 katika Mkoa wa kigoma.


Post a Comment

0 Comments