Ticker

6/recent/ticker-posts

KATAMBI: SERIKALI YAJIPANGA KULINDA HAKI YA MWAJIRI NA MWAJIRIWA KAZI ZA MTANDAONI


Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi,akizungumza kwenye kongamano la Jumuiya ya Sheria za Kazi Tanzania lililolenga kujadili masuala yanayohusu uchumi wa mtandaoni.

Na Mwandishi Wetu.

Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema serikali imeanza kufanya utafiti wa mfumo mpya wa kufanya kazi kwa njia ya mtandao ili kuja na sera itakayoendana na sheria za kazi katika kulinda haki za mwajiri na mwajiriwa.

Mhe. Katambi amesema hayo kwenye kongamano la Jumuiya ya Sheria za Kazi Tanzania lililolenga kujadili masuala yanayohusu uchumi wa mtandaoni ili kuendana na mfumo wa kisasa wa kidunia unaotokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambao unawataka watu kufanya kazi kwa njia ya mtandao.

"Tunayo sheria ya ajira ya mahusiano kazini lakini pia tuna sera ya ajira na taratibu nyingine ambapo sasa kwa hawa wanaofanya kazi kwa njia mtandao bado ni jambo jipya, hivyo tunaangalia namna gani haki zote hizo zitalindwa," amesema Mhe.Katambi.

Amesema haki zitakazozingatiwa ni masuala ya muda wa kazi, mifumo ya kuajiriwa kwa mikataba ya kudumu na ya muda mfupi, jinsi ya kutoa huduma, uwezo wa utendaji kazi wa mfanyakazi, usalama mahali pa kazi na michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii katika ngazi aliyoajiriwa.

Pia, amesema mfumo huo utaangalia ulipaji wa mishahara na mifumo ya malipo, ulipaji wa kodi za serikali, haki za mfanyakazi kwenye likizo na saa za kufanya kazi kwasababu mfumo huo ni tofauti na uliopo kwa sasa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya sheria za kazi nchini, Deogratius Kilawe amesema mfumo huo utasaidia kuleta mabadiliko katika sekta ya uchumi nchini na kuwatambua waajiri na waajiriwa kisheria.


Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi,akizungumza kwenye kongamano la Jumuiya ya Sheria za Kazi Tanzania lililolenga kujadili masuala yanayohusu uchumi wa mtandaoni


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa kongamano la Jumuiya ya Sheria za Kazi Tanzania lililolenga kujadili masuala yanayohusu uchumi wa mtandaoni


Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kongamano la Jumuiya ya Sheria za Kazi Tanzania lililolenga kujadili masuala yanayohusu uchumi wa mtandaoni

Post a Comment

0 Comments