Ticker

6/recent/ticker-posts

KCB BANK NA WIZARA YA ELIMU KUSHIRIKIANA KATIKA MRADI WA KUENDELEZA VIJANA 5,000 KIUJUZI NCHINI TANZANIA

Benki ya KCB Tanzania na Wizara ya Elimu wamefanya mazungumzo ya uwezekano wa kushirikiana katika mradi wa kuwawezesha vijana 5,000 kiujuzi nchini Tanzania ambapo Wizara hiyo inaona umuhimu wa ushirikiano ili kuhakikisha vijana wengi zaidi wanafanikiwa.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika Septemba 14 wizarani - Dodoma yalilenga kuangalia maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili ili kufanikisha mradi huo. Mafunzo hayo yanadhaminiwa na Benki ya KCB Tanzania kupitia vyuo mbalimbali vya ufundi ikiwamo VETA, SIDO na Vyuo vya Maendeleo (FDC).

Profesa Adolf Mkenda aliipongeza Benki ya KCB Tanzania kwa kuja na mradi ambao una manufaa makubwa kwa Taifa kwani uhitaji bado ni mkubwa sana.

Katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Technologia, Prof. Carolyne Nombo aliipongeza Benki ya KCB kwa jitihada inazofanya katika kuwainua vijana hususani katika kuongeza ujuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa KCB Bank ChristinaManyenye alisema mradi huo unatarajia kuanza mwezi Septemba na utafanyika katika Mikoa sita (6) ikiwamo Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Shinyanga, Arusha na Kilimanjaro. Pia, mradi huu utafanyika visiwani Zanzibar (Unguja na Pemba).

“Tunapenda kuishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinoogia kwa kulipokea vizuri jambo hili ambalo lina manufaa kwa maendeleo ya vijana hapa nchini. KCB Bank tunaamini kwamba tukiwapa mafunzo vijana wanaweza kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi kupitia kujiajiri,” alisema Manyenye na kusisitiza kwamba program hii ni endeleve.

Benki ya KCB Tanzania ni mdau wa maendeleo na imekuwa ikitekeleza mradi wa 2jiajiri toka mwaka 2016 na hadi sasa mradi huo umewanufaisha watanzania zaidi ya 1,500 kwa kuwapa mafunzo ya ufundi stadi na kuwawezesha kuanzisha biashara mbalimbali. Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinologia, Profesa Adolf Mkenda akizungumza na viongozi wa KCB Bank Tanzania, Christina Manyenye, Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano (wa tatu kulia) na Betty Muruve, Meneja wa Mradi wa KCB 2jiajiri,(wa pili kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinologia, Prof. Carolyne Nombo na Kamishna wa Elimu, Dk. Lyabwene Mtahabwa. Mazungumzo hayo yalilenga kujadili maeneo ya ushirikiano katika mradi wa kuwawezesha vijana 5,000 kiujuzi nchini unaofadhiliwa na benki ya KCB Tanzania.

Post a Comment

0 Comments