Ticker

6/recent/ticker-posts

MAAFISA UVUVI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO YA SHERIA YA UTUNZAJI WA WANYAMA BAHARI YA MAREKANI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WATAALAMU wa Uvuvi kutoka Tanzania Bara na Visiwani wameanza Mafunzo ya kujengewa uwezo kwenye masuala ya Sheria ya Utunzaji wa Wanyama bahari ya Marekeni ambayo yanatolewa na Wataalamu wabobezi kutoka nchini Marekani.
Akizungumza na Waandishi wa habari wakati akifungua Mafunzo hayo leo Septemba 11,2023 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amesema Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinauza mazao ya bahari pamoja na mazao hai kutoka baharini na wanauza mazao hayo hadi Marekeni.

"Wao Marekani ili ufanye nao biashara lazima ufahamu sheria zao, kupitia Shirika la Kimataifa la USAID waliona ni vizuri walete wataalamu ili wawafundishe maafisa Uvuvi wa Tanzania". Amesema

Aidha Prof. Shemdoe amesema mafunzo hayo namna mojawapo ya kulitangaza soko la mazao ya uvuvi katika nchi yetu ya Tanzania ambapo itafungua mwanya wa kupata wawekezaji wakubwa katika sekta ya mazao ya wanyama bahari.

Pamoja na hayo amewasisitizia maafisa hao wazingatie mafunzo hayo wanayopewa kwasababu sio wote uhudhuria mafunzo hayo ya mazao bahari hivyo wawe mabalozi na wakufunzi kwa wengine ambao hawakufika katika mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku tano ambapo yameanza leo Septemba 11,2023 na kufikia tamati Septemba 15,2023.

Post a Comment

0 Comments