Ticker

6/recent/ticker-posts

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WAHITIMU VYUO VIKUU NCHINI KUANZA SEPTEMBA 25,2023

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) inatazamiwa kuwafikia vijana wahitimu takribani 1,200 katika Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu Vya Elimu ya Juu Tanzania ambayo yanatarajia kuanza Septemba 25 hadi Oktoba 12,2023 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Katika Mikoa mingine ya Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kigoma, Lindi, Kusini Pemba na Mjini Magharibi mafunzo hayo yataanza Oktoba 16 hadi 20,2023.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Septemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ubunifu na Ujasiriamali, Prof. Hannibal Bwire amesema mafunzo hayo yanalenga kuwapatia vijana uelewa, taarifa, maarifa, Ujuzi na uwezo wa kuainisha fursa zinazowazunguka na kuweza kuzitumia fursa hizo kwa kuanzisha ajira kwa ajili yao na wenzao na hivyo kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla.

"Utoaji wa Mafunzo haya ni mojawapo ya harakati za UDSM katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kutatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana hapa nchini". Amesema Prof.Bwire

Aidha amesema kuwa washiriki watapata fursa ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wa biashara na kuungana na taasisi za Serikali na binafsi zinazotoa huduma kwa wajasiriamali kama vile SIDO, TBS, TRA, BRELA, TANTRADE, Manispaa za mikoa husika na baadhi ya washiriki waliokwishapata mafunzo hayo mwaka 2019, 2021 na 2022.

Amesema Mafunzo yatatotolewa katika makundi ya watu wasiozidi 50 kwa darasa,na washiriki wa mafunzo hayo watajigharamia usafiri na malazi na gharama nyingine zitagharamiwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

"Tunawahimiza washiriki wanaopenda kujiunga na mafunzo haya kujisajiri kujaza fomu ya maombi iliyo mtandaoni kwenye tovuti ya udsm-gep.ac.tz/ na kwa mwaka huu tunahamasisha vijana na vikuundi walio hitimu Elimu ya juu na ambao hawana Elimu ya juu fursa hii imetolewa tu kwa mikoa ya Dar es Salaam,Iringa na Lindi"Amesema.

Kwa upande wake Mratibu-Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Winnie Nguni amesema mafunzo hayo yanalenga kumuimarisha kijana kuweza kutengeneza bidhaa ambayo itauzika na kuweza kumfikisha katika mahala ambapo anaweza kusaidia na wengine kupitia biashara yake.

Dkt.Winnie amesema mpaka sasa wamehudumia Zaidi ya Vyuo 70 na katika mikoa mingi vijana wengi wana uhitaji wa mafunzo hayo.

"Kijana akiwa na biashara yake akiendesha kisomi mafanikio yake ni makubwa kuliko yule ambaye hakupata nafasi ya kusoma elimu ya juu"Amesema.

Nae Mwezeshaji wa Mafunzo ya Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Biashara, Dkt.Theresia Busagara amesema kupitia mafunzo hayo chuo kina kuwa kimetoa fursa nzuri ya usimamizi wa fedha hivyo kuwa rahisi kwa urejeshaji wa mikopo na usimamizi wa kifedha kwa wahitimu wa mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yamebeba kauli mbiu isemayo "BADILI CHANGAMOTO KUWA FURSA",iliyo lenga kubadiri Mtizamo wa Vijana ili kuziona changamoto na kuzigeuza kuwa Fursa.

Mkurugenzi wa Ubunifu na Ujasiriamali, Prof. Hannibal Bwire akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea katika Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu Vya Elimu ya Juu Tanzania hivi karibuni.
Mratibu-Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Winnie Nguni akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea katika Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu Vya Elimu ya Juu Tanzania hivi karibuni.

Mwezeshaji wa Mafunzo ya Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Biashara, Dkt.Theresia Busagara akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea katika Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu Vya Elimu ya Juu Tanzania hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments