Ticker

6/recent/ticker-posts

"NAWAPONGEZA KWA HATUA ILIYOFIKIWA KWENYE UJENZI WA OFISI" -KIGAHE

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe(MB) amepongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la ofisi ya Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO).

Mheshimiwa Kigahe amefanya ziara ya Kikazi ikiwa ni utaratibu wake wa kutembelea miradi ya Maendeleo katika taasisi mbalimbali zilizo chini Wizara yake ya Viwanda na Biashara.

‘’Kwa kweli leo nimefurahi kuona kazi inaendelea vyema, niwapongeze SUMA JKT lakini pia TIRDO kwa usimamizi mzuri wa ujenzi’’ aliongeza Mhe.Kigahe.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda(TIRDO) Prof.Mkumbukwa Mtambo alimueleza Naibu Waziri kuwa kwa sasa wanaridhishwa na hatua iliyofikiwana Mkandarasi ambapo amesema wanatarajia kuhamia kwenye jengo hilo jipya katika mwaka huu wa fedha 2023/2024.

‘’Mheshimiwa Naibu Waziri tunashukuru kwa ushirikiano mkubwa kutoka Wizarani na tunatarajia kuhamia jengo letu jipya jambo litakaloongeza motisha na hari ya kazi kwa wafanyakazi’’ aliongeza Prof. Mtambo.

Prof. Mtambo pia alitumia nafasi hiyo kumueleza Naibu Waziri uweza wa kitaalam wa Shirika baada ya kuwezeshwa na Serikali ambapo kwa sasa Shirika lina maabara za kisasa za sekta mbalimbali kama vile maabara ya Ngozi,Maabara ya nishati, Maabara ya Chakula Pamoja na maabara ya madini.

Prof.Mkumbukwa amemueleza naibu Waziri kuwa uwepo wa maabara hizo utaongeza ufanisi wa taasisi katika kuwahudumia wananchi lakini pia kutatua chngamoto zilizopo katika Sekta za uzalishaji na Viwanda nchini.

Jengo la ofisi ya Makamu Makuu ya TIRDO linajengwa na Mkandarasi ambaye ni Shirika la Uzalishaji Mali la JKT (SUMA JKT) ambapo kwa sasa limefika katika hatua ya umaliziaji (finishing).


Post a Comment

0 Comments