Ticker

6/recent/ticker-posts

BOTRA WATOA MSAADA KITUO CHA WAZEE NUNGE KIGAMBONI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHAMA cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA), wametembelea na kutoa msaada katika kituo cha Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha Wiki ya Wazee Duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo leo Oktoba 7,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa BOTRA, Bi. Mwenyekiti Grace Rubambey amesema wamekutana kwa pamoja na kuona kuna umuhimu wa kusheherekea pamoja na Wazee wa kituo hicho na kuzungumza na kushauriana mambo mbalimbali ya kijamii.

“Sisi wazee tunachangamoto, kila mmoja hapa anachangamoto yake, tumekutana pamoja na wazee wenzetu katika kituo hicho na kuzungumza mambo mbalimbali na kushauriana na pia tukaona na umuhimu wa kuwaletea kitoweo, chakula na vitu mbalimbali kulingana na mahitaji yao”. Amesema

Aidha amesema kuwa kutokana na malengo waliojiwekea Chama, wameona itakuwa vizuri kuwatembelea wazee wenzao siku hii ya leo ili kusherehekea Siku Kuu ya Wazee ulimwenguni, kubadilishana mawazo na kupeana mtumaini.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi Makazi ya Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Bi.Jacklina Kanyamwenge ameishukuru Chama hicho kwa kuweza kuwatembelea na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo Vyakula, mashuka, mafuta ya kupaka pamoja na vitu vingine ambavyo vitakuwa na msaada mkubwa kwa wazee kwenye kituo hicho.

Amesema kituo hicho kina wazee takribani 21, wanawake 11 pamoja na wanaume 10 ambapo wamekuwa wakiwapata kupitia manispaa wakiwa wanaangali sifa mojawapo awe ni Mtanzania na awe amekosa matunzo kwenye jamii na wanawapata kupitia maafisa ustawi wa jamii.

Hata hivyo amesema katika kituo hicho ambacho kipo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu kuna mahitaji yote ya kijamii ikiwemo zahanati ambayo inahudumia pia jamii ambayo inawazunguka.

Mwenyekiti wa BOTRA, Bi. Mwenyekiti Grace Rubambey akikabidhi mashuka na mafuta ya kupaka kwa mmoja wa wazee katika Kituo cha Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati walipowatembelea wazee kwenye kituo hicho leo Oktoba 7,2023.
Makamu Mwenyekiti wa BOTRA Bw.Leonard Kisarika akikabidhi mashuka na mafuta ya kupaka kwa mmoja wa wazee katika Kituo cha Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati walipowatembelea wazee kwenye kituo hicho leo Oktoba 7,2023.
Wanachama wa Chama cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) wakikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wazee katika Kituo cha Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati walipowatembelea wazee kwenye kituo hicho leo Oktoba 7,2023.
Mwenyekiti wa BOTRA, Bi. Mwenyekiti Grace Rubambey pamoja na Makamu wake Bw.Leonard Kisarika wakizungumza na mmoja wa wazee Bw.Mohammed Ally wakati walipotembelea Kituo cha Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati walipowatembelea wazee kwenye kituo hicho leo Oktoba 7,2023 Jijini Dar es Salaam

Wanachama wa Chama cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) wakizungumza na wazee wakati walipotembelea Kituo cha Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 7,2023
Mwenyekiti wa BOTRA, Bi. Mwenyekiti Grace Rubambey akizungumza wakati walipotembelea na kutoa msaada katika Kituo cha Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 7,2023 wakati wakiadhimisha Wiki ya Wazee Duniani.

Afisa Mfawidhi Makazi ya Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Bi.Jacklina Kanyamwenge akizungumza wakati akiwakaribisha wanachama wa Chama cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) walipotembelea kituo hicho leo Oktoba 7,2023 na kutoa msaada wakati wakiadhimisha Wiki ya Wazee Duniani.
Wanachama wa Chama cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) wakiwa wamebeba vyakula na baadhi ya vitu kwaajili ya kutoa msaada katika Kituo cha Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wakati wakiadhimisha Wiki ya Wazee Duniani leo Oktoba 7,2023
Wanachama wa Chama cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA wakiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wakati walipotembelea Kituo cha Wazee wasiojiweza Nunge Kigamboni Jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wakati wakiadhimisha Wiki ya Wazee Duniani leo Oktoba 7,2023


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments