Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT.HASHIL- DKT SAMIA AMEBORESHA MAZINGIRA MAZURI YA BIASHARA NCHINI


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara  Dkt Hashil Abdallah amesema Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan anahakikisha mazingira ya uwezeshaji wa biashara nchini ni mzuri ikiwa ni pamoja na kuhakikisha muda na gharama za kufanya biashara ni rafiki kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.

Ameyasema hayo leo Oktoba 21,2023 alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kikao chenye lengo la kuzungumzia uwezeshaji wa biashara na uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini,katika Ukumbi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) jijini Dar es Salaam.

Amesema "tunapozungumzia biashara ya kimataifa lazima uzungumzie vitu vitatu ambavyo ni kuuza nje ya nchi,kununua kutoka nje ya nchi ,kusafirisha kwenda nje nchi,hivyo tutaangazia yanayohusu kufanya biashara ndani ya mipaka ya nchi na biashara zinazovuka mipaka ya nchi ili kuweka mazingira bora ya biashara.

Aidha Dkt. Hashil amesema ili mafaniko yaonekane na kufanya tathimini lazima kuwepo na mkakati elekezi na lazima kamati ya uwezeshaji wa mazingira bora wakutane ili kutoa maadhimio kwa pamoja ili kurahisisha mazingira ya biashara.

"Jukumu la Serikali ni kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara, tunaenda kuangalia wajibu wetu kupitia mkataba wa kimataifa wa WTO ambao sisi kama nchi tumekutana ili kutimiza malengo ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu ndio maana leo Kuna watu zaidi ya 100 kutoka sekta binafsi na umma kama Bandari,Uhamiaji,PSPF na TBS,Wizara ya fedha ili kama kuna Changamoto tuzitatue kwa pamoja ili tuokoe muda wa ufanyaji biashara na tuokoe gharama za kufanya biashara" Amesema.

Post a Comment

0 Comments