Ticker

6/recent/ticker-posts

NIDHAMU YAMPA SHAVU BONDIA MANDONGA

NA MWANDISHI WETU

BONDIA wa Ngumi za Kulipwa nchini Karim Mandonga 'Mtu kazi' alamba dili kampuni ya Mr.Discount Hyper Market kupitia chapa ya utengenezaji viatu ya "Relaxo .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 21,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa kumtangaza ubalozi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mr. Discount Hyper Market Bw.Khalid Mubarak amesema sababu ya kumchagua Mandonga na nidhamu yake katika jamii na kufanya vizuri katika mchezo wa masumbwi nchini.

"Mandonga amekuwa bondia mwenye nidhamu ambapo kama kampuni tumeona tuongeze nguvu ya kuweza kusaidia kuwafikia wateja wetu mbalimbali kwa bidhaa zetu bora za viatu. " Amesema Bw.Mubarak.

Hata hivyo Mubarak ameeleza kuwa Kampuni ya Mr. Discount Hyper and supermarket wametoa nafasi ya wadau wa michezo kupendekeza majina ya wanamichezo wengine kwa upande wa riadha na mpira wa miguu kuwa sehemu ya Ubalozi wa kampuni hiyo.

Kwa upande wake Karim Mandonga amesema ni wakati wa mabondia kujitafakari na kuendesha michezo hiyo katika hali ya kinidhamu ili makampuni yaweze kujitokeza kuwapa nafasi ya kuwakilisha makampuni na bidhaa zao ( ubalozi).

"Tunaelewa changamoto zinazotukabili wanamichezo ikiwemo uhakika wakuwa na vifaa vya mazoezi hivyo kuwepo kwa wadau kama 'Mr.Discount ' inatupa morali ya kufanya vizuri katika michezo yetu."
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mr. Discount Hyper Market Bw.Khalid Mubarak akizungumza na waandishi wa habari wakati akimtangaza Karim Mandonga kuwa balozi wao mpya leo Oktoba 21,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Utengezaji Viatu Relaxo, Bw. Mosheer Ahmad akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kumtangaza mwanamasumbwi Karimu Mandonga kuwa balozi mpya wa Kampuni ya Mr. Discount kupitia Chapa ya utengenezaji wa Viatu ya Relaxo leo Oktoba 21,2023 Jijini Dar es Salaam
Bondia wa Ngumi za kulipwa nchini Karim Mandonga akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa balozi wa kampuni ya Mr.Discount Hyper Market kupitia chapa ya utengenezaji viatu ya "Relaxo leo Oktoba 21,2023 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments