Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA PAMOJA NA MGENI WAKE RAIS WA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA UJERUMANI WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier nchini Tanzania. Mkutano huo na Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu ziara yake nchini Tanzania. Mkutano huo umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.
Wageni mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier pamoja na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier wakati wa Mkutano wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujerumani uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki katika Kongamano la Wafanyabiashara kati yao na Ujerumani lililofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.
Sehemu ya Ujumbe wa Ujerumani ulioshiriki katika Kongamano la Wafanyabiashara kati yao na Tanzania lililofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier wakati wa Mkutano wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujerumani uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.

Post a Comment

0 Comments