Ticker

6/recent/ticker-posts

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA TEKNOLOJIA KUJIENDELEZA

12 Oktoba 2023, Morogoro

——————————————————

Katibu Mkuu wa Chama Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), Komredi Hery Mkunda, amewataka vijana kutumia Fursa ya Maendeleo ya Teknolojia kujiletea maendeleo binafsi pamoja na maendeleo ya Chama kwa Ujumla pia kutumia fursa hio kutafuta fursa za masomo na mafunzo.

Komredi Mkunda ameyasema hayo leo Alhamisi tarehe 12 Oktoba 2023, Mkoani Morogoro alipokuwa Mgeni Rasmi katika Semina kwa wawakilishi wa Vijana -TUGHE yenye lengo la kuwajengea uwezo Viongozi wa Vijana ili kuwa chachu ya mabadiliko katika maeneo yao ya kazi na jamii kwa ujumla.

Pia Katibu Mkuu ametumia Semina hio kuwataka vijana kuweka mikakati mizuri itakayosaidia kuongeza wanachama wapya pia vijana kujitoa na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ambazo zitasaidia kukitangaza Chama.

Sambamba na hayo pia amewaasa vijana kujituma na kufanya kazi zao kwa weledi ili waweze kuaminiwa na kupewa majukumu makubwa zaidi na pia amewaonya kuacha tabia ya kulalamika panapokuwa na changamoto na badala yake wawe watu wa kutoa majibu na suluhisho.

Semina hii imehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Vijana Taifa pamoja na wawakilishi wa Vijana kutoka mikoa mbali pamoja na Viongozi mbalimbali wa TUGHE kutoka Mkoa wa Morogoro pamoja na Makao Makuu.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Vijana Taifa, Ndugu Dominicus Nyoni kwa niaba ya Vijana amemkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa TUGHE kama ishara ya kumpongeza kwa kazi nzuri ya kukiongoza vema Chama cha TUGHE na kumtakia heri katika uongozi wake.

Semina hii imekuja wakati ambapo tunaelekea katika maadhimisho ya wiki ya Vijana ambayo kilele chake kitafanyika Jumamosi hii Oktoba 14, Mkoani Manyara ambapo kwa mwaka huu yamebeba kaulimbiu inayosema “Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo endelevu”

“Huduma Bora, Maslahi Zaidi”

Post a Comment

0 Comments