Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAWAKE WAASWA KUEPUKA KUTOA MIKOPO SEHEMU NYINGI ILI KUYAMUDU MAREJESHO


*************

Na Shemsa Mussa,Kagera.


Akina mama wamehaswa kuepuka kutoa mikopo sehemu nyingi ili kumudu uwezo wa marejesho ikiwa baadhi wameyakimbia makazi yao kwa kukosa pesa za kurejesha kwenye vikundi .

Akizungumza katika kikao cha Buwea Saccos kilichofanyika katika ukumbi wa karumco Halmashauri ya Bukoba Bi Regina Majaliwa Mwenyekiti Buwea amesema kuwa lengo la kuanzisha chama hicho cha ushirika ni kuwasaidia na kuwainua wanawake kiuchumi.


Amesema mpaka sasa wanawake wamekuwa wakitangatanga kuchukua mikopo sehemu tofauti na kubadilisha mtazamo wa kuwasaidia na kuanza kuhangaika kufikilia ni wapi watatoa marejesho ya mikopo waliyonayo na baadhii yao kuzikimbia familia zao na kuwasihi kujenga uhaminifu pindi wanapochukua mikopo kwa sababu shida haziishi.


"Nawaza kila siku kwa ajili yenu nyie wanawake na afya yangu inazorota nahisi ni nyie mimi natamani kila mwanamke awe na maendeleo aweze kuisimamia hata familia yake bila kutegemea sehemu yoyote ndio maana mwanzo kabisa tulianza kwa kuwapa mifugo ili mzalishe mpate pesa ,ukioa pesa ya kikundi basi rejesha ila sio kukimbia kumbuka shida haziishi kila siku zipo,amesema Majaliwa"


Aidha nae Bi Grace Mushongi ambaye ni moja ya wanufaika wa Buwea Saccos amesema kuwa changomoto nyengine inayopelekea wanavikundi kutorejesha mikopo ni viongozi kukaa kwenye uongozi ( madaraka )kwa muda mrefu matokeo yake kunajengwa mazoea kati yao na kupelekea kuddharau na kutorejesha mikopo pia ameshauri kutompatia mkopo mtu aliyechukua mikopo sehemu nyingine.


Nae Katibu wa Mkutano huo Bi Odetha Alexander amesema katika Saccos yao wamekuwepo washirika wanaoshindwa kurejesha pesa na wadaiwa sugu kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuuguza kwa muda mrefu ,vifo pamoja na hali ya maisha kuwa mbaya kupelekea baadhi ya wanaume kutelekeza familia na kupelekea wanawake kuchukua jukumu la kulea familia pekee.


Pia Bi Adventina Byera Mwenyekiti wa kikundi Tawi la Bujugo amewashauri wanawake kupanda miti ili kutunza mazingira na kutafuta vyanzo tofauti tofauti vya kuongeza mapato huku akiwashauri kujikita katika kilimo cha Alzeti ,Vanila na parachichi ili kuendelea kujiinua kiuchumi .


Hata hivyo, nae Mgeni rasmi katika kikao hicho Bw Obadia Kyakajumba Afisa ushirika Manispaa ya Bukoba ameanza kwa kuipongeza bodi kwa jitihada za kufanya mkutano huo na kusema mkutano ni sehemu ya kujadili mambo mengi na kujenga chama pia amesema Saccos ni chama cha ushirika cha kuweka na kukopa na ushirika wowote lazima kuwepo kiingilio,hisa na Akiba.


Kikao hicho kimejadili na kupendekeza kuongeza hisa kutoka shilingi 2000 iliyokuwepo awali na kuchanga shilingi 10000 kwa kila Mwanachama

Post a Comment

0 Comments