Ticker

6/recent/ticker-posts

CCWWT YATOA TAMKO JUU YA UKATILI ALIOFANYIWA KIJANA HASHIMU NA MBUNGE


Na Hamida Kamchalla, ARUSHA.

CHAMA Cha Wazee Wanaume Tanzania (CCWWT) kimelaani vikali kitendo cha ukatili alichofanyiwa kijana Hashimu Ally aliyekuwa mfanyakazi wa Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul, aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria kabla ya kutenguliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Kiongozi mkuu wa CCWWT Taifa Tadey Mchena amesema wanatarajia kufanya ziara nchi nzima kupinga na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia na kudai kuwa viongozi wote wanapaswa kuzingatia viapo vya maadili ya Uongozi na Utawala Bora.


"Tunapinga vikali kitendo hiki na endapo tuhuma hizi za Mh. Gekul zitathibitika ni unwell basi tunashauri hatua kali zichukuliwe dhidi yake ili iwe funzo kwa wengine" amesema Mchena.


Aidha Mchena amesema CCWWT kinampongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kumtengua mbunge huyo kwani tuhuma zinazomkabili ni jambo ambalo kama kiongozi anastasia kuigwa lakini siyo kupotosha umma.


"Tumemuelwwa sana mama yetu kwa utenguzi wake, tunampongeza pia kwani hapa ameonesha ujasiri na uongozi wake kwa cheo chake, tunaomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa haraka ili sheria ifuate kulingana na kitendo hiki" amebainisha.


Hata hivyo Mchena alieleza kwamba CCWWT inatoa pole kwa familia pamoja na kijana Hashimu kutokana na kitendo alichofanyiwa huku ikimtaka kuwa mtulivu wakati ikisubiriwa uchunguzi kukamilika.


"Tunampa pole kujana wetu na kumsihi awe mtulivu ingawa ni wazi kwamba ameathiriwa na anahitaji msaada wa saikolojia lakini pia tunaiomba familia iendelee kumfariji na kumuondoa katika hali ya mashaka" amesema.


Picha. Kiongozi wa Chama Cha Wazee Wanaume Taifa Tadey Mchena.

Post a Comment

0 Comments