Ticker

6/recent/ticker-posts

HONGERA KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA SERIKALI YAKE KWA UBUNIFU

   

 Na Nyabaganga Taraba - Iringa.


Kamati ya kudumu ya bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali kwa ubunifu utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipotembelea Skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi iliyoko Iringa Tarafa ya Pawaga.


Skimu ina ukubwa wa hekta 6000 na wanufaika wa skimu hiyo ni watu elfu kumi na sita (16,000) wa Vijiji sita (6) vya Kata mbili za Itunundu na Mloli, gharama za ujenzi wa mradi ni kiasi cha shilingi Bilioni 59 fedha za kitanzania.


Mwenyekiti wa kamati ya bajeti amewataka wananchi wa Tarafa ya Pawaga kutunza mradi ili uwe endelevu maana wanufaika ni wao.


Mhe. Daniel Sillo amesema lengo la ziara hiyo ni kujionea fedha zilizopangwa na Bunge na kupelekwa Wizara ya kilimo kwa ajili ya miradi zimefanya kazi gani,amesema wamejionea na hawana wasiwasi na kinachoendelea katika miradi hiyo. Hivyo walichokiona na taarifa waliyoipata watazitumia kushauri Serikali.

Wanakamati nao kwa nyakati tofauti wamewataka wananchi wa pawaga kutunza hiyo neema ambayo italeta mabadiliko makubwa kwa wakulima na nchi kwa ujumla.


Akitoa shukrani zake Mwenyekiti wa skimu hiyo inayojengwa ya Mkombozi ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani kwa kusikia kilio chao cha siku nyingi. Eneo la Pawaga ni kame hivyo skimu hii ni msaada mkubwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji amesema Tume bado ina mpango wa kuendeleza zaidi skimu hiyo kwa maana ya kujenga bwawa la kuhifadhi maji ili wakulima waweze kulima zaidi ya mara moja kwa mwaka na kuongezea tija ya mradi huo mkubwa wa kilimo cha mpunga.

Akipokea maoni ya kamati Naibu Waziri wa kilimo Mhe. David Silinde amesema “haya yanayoonekana katika mradi huu, ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba kila eneo linalofaa kilimo cha umwagiliaji liwekewe miundombinu ya umwagiliaji ili wananchi watoke kwenye kilimo cha asili walime kisasa. Amesema Silinde.

Aidha, ameiambia kamati hiyo ushauri uliotolewa na hakamati utafanyiwa kazi na hakuna litakaloachwa. Amewataka wananchi wa Pawaga kulinda mradi maana ndio wanufaika.

Pamoja na hayo amesema wakati wowote kuanzia sasa miradi mingine mia moja (100) itatangazwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wake maeneo ya mbalimbali hapa Nchini.

 

Agenda 10/30 kilimo ni biashara.


Post a Comment

0 Comments