Ticker

6/recent/ticker-posts

HUWEZI KUTENGANISHA JIJI LA DAR NA SOKO LA KARIAKOO’ MCHENGERWA

OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema ameridhishwa na ukarabati na ujenzi wa Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Ameyasema hayo Novemba 15,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa Jengo la Soko Kuu la Kariakoo.

“Nichukue fursa hii kupongeza uongozi wa kwa usimamizi wa soko hili la Kariakoo,lakini na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Mhe. Mama Ghasia.

“Lakini, pia nimpongeze Mkuu wa Mkoa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, kwa usimamizi mzuri wa soko hili ambalo ndiyo kitovu cha Dar es Salaam.

“Unapoizungumzia Dar es Salaam, unaizungumzia Kariakoo na Soko la Kariakoo lina historia kubwa sana.

“Lazima tumshukuru na kumpongeza sana Rais wetu Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha takribani shilingi bilioni 28 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu wa soko la Kariakoo ambalo ni soko lenye historia pan sana ya nchi yetu Tanzania.

“Lakini, pia unapolizungumzia Jiji la Dar es Salaam unalizungumzia Soko la Kariakoo, kwa hiyo tunampongeza sana Mheshimiwa Rais.

“Leo tumefanya ukaguzi na nimeridhika kwamba, ujenzi unakwenda vizuri na takribani asilimia 85 imekwishatekelezwa.

“Na sisi tunaamini kabisa kwamba Mkandarasi kufikia mwezi wa pili mwakani atakuwa amemaliza na tutamuomba Mheshimiwa Rais yeye mwenyewe aje awakabidhi wananchi.

“Watanzania, wananchi wa Dar es Salaam soko hili la Kariakoo, kwa hiyo nimeridhika na ujenzi.Na ndiyo maana nachukua fursa hii kuwapongeza sana wasimamizi, nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu wa Mkoa kwa ufuatiliaji wa karibu, kuja mara kwa mara.

“Lakini, pia kufuatilia kuhakikisha kwamba thamani ya fedha iliyotolewa na Mheshimiwa Rais inakwenda kukidhi malengo ambayo Mheshimiwa Rais ameyakusudia katika ujenzi wa soko la kisasa kabisa la Kariakoo ambalo sasa limeongezwa mara dufu, tofauti na pale lilipokuwa awali.

“Sasa hivi, kutakuwa na maduka mengi, migahawa mingi, na maeneo mengi ya uchuuzi ambayo Watanzania wataweza kuyatumia wakati wa soko hili la Kariakoo.

“Kwa hiyo, tumshukuru Mheshimiwa Rais na mimi niendelee kumuomba Mkandarasi anayetekeleza mradi huu kuhakikisha vile viwango ambavyo Serikali imevikusudia wakati anamalizia utekelezaji wa mradi huu basi kisipungue kiwango hata kimoja.

“Maana yake ni kwamba tunagegemea tupate soko la kisasa zaidi, wakati wa umaliziaji wa utekelezaji wa mradi huu.

Post a Comment

0 Comments