Ticker

6/recent/ticker-posts

MHE. KIKWETE AZINDUA ZOEZI LA USAMBAZAJI WA MFUMO WA KUTATHMINI NA KUHAKIKI UTENDAJI KAZI

Uzinduzi wa Zoezi la Usambazaji wa mfumo wa kutathmini na kuhakiki utendaji wa kazi wa Watumishi na Taasisi yaani PEPMIS/PIPMIS NA HR Assessment limefanyika mapema tarehe 20 Novemba 2023 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, mjini Iringa.

Akizungumza wakati anazindua mpango huo wa usambazaji wa Mfumo wa PEPMIS/PIPMIS NA HR Assessment katika shughuli ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Bibi Halima Dendegu, Katibu Tawala wa Mkoa huo Mwandisi Masanja, na watumishi mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoa huo na waratibu wa TASAF toka makao makuu ya TASAF -Dodoma ambao walifuatana na Naibu Waziri ; Mh. Kikwete aliuelezea mfumo huu kuwa unakwenda kutatua pamoja na changamoto nyenginezo katika utumishi, mapungufu yaliyojitokeza katika mfumo wa OPRAS. Ndugu Naibu Waziri aliwakumbusha watumishi kujua kuwa mfumo huu imekuja kuleta ufanisi na faida nyingi ikiwemo kutambua mahitaji ya kweli ya kiutumisi katika ofisi za umma na kuwahudumia Wananchi.

Post a Comment

0 Comments