Ticker

6/recent/ticker-posts

UZINDUZI WA KIKUNDI KAZI CHA MAPINDUZI YA KIDIGITALI (DTWG)

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Biashara (TNBC) wamezindua kikundi kazi cha Mapinduzi ya Kidigitali (DTWG) maalumu kushughulika katika masuala ya Tehama kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanatumia Tehama katika kufanya manunuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Nov 6,2023 wakati wa hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha DTWG Bw. Mohammed Abdulla amesema kuwa wanatarajia kurahisisha huduma ambapo wanatarajia kuwepo na uunganishwaji wa mifumo kupitia kitambulisho cha taifa na kuokoa muda.

"Hatuna sheria ya masuala ya TEHAMA nchini, sisi kama Wizara tumeona tuanze na sera ambayo tunayo ya 2006 ambapo tutaihuisha kisha tuje na sheria ambayo utagusa kote sekta binafsi na ya Umma"Amesema.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa TNBC, Dkt. Godwil Wanga amesema kuwa yanafanyika maboresho makubwa ambayo yataleta tija katika uchumi wa kidigitali nchini na wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi.

"Tunakuja na maboresho ambayo yataleta tija, wapo wajumbe wetu ambao ni wa sekta ya umma na binafsi wanaujuzi wamesomea hivi vitu kwani nisehemu ya kazi yao katika utendaji wa kila siku,tunajua nchi ambazo zimefanya vizuri katika mapinduzi ya kidijiti hata wataalamu ambao wameteuliwa na katibu kiongozi wamehusika hata kwenda huko nje kusoma na kuelewa hivyo tunaaminj wateleta mchango katika maendeleo"Amesema

Pamoja na hayo amesema kuwa katika kushiriki mkutano wa kimataifa wapo watu ambao wako tayari kuwekeza nchini kwa ajili ya uzalishaji wa simu Janja ambapo itasaidia wananchi kupata simu hizo kwa bei rahisi.

Naye Mwakilishi wa Sekta binafsi Bi. Jackline Mwaisu amesema Sekta binafsi itatoa mchango mkubwa katika kuendeleza masuala ya kidijitali katika eneo la kibiashara katika sekta mbalimbali za biashara, kama kilimo kupata bei za bidhaa na taarifa za biashara pamoja na kufanya malipo.

Katika tukio lingine ambalo limefanyika leo katika hafla hiyo ni kushuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya mradi wa Tanzania ya Kidijitali yenye thamani ya sh. bilioni 43.3.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha DTWG, Mohammed Khamis Abdulla akizungumza wakati akifungua Kikao Maalum cha Kwanza cha Kikundi Kazi cha Mapinduzi ya Kidijitali (Digital Transformation Working Group) cha TNBC, ukumbi wa TCRA, jijini Dar es Salaam, Tarehe 06 Novemba, 2023.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha DTWG, Mohammed Khamis Abdulla akisisitiza jambo wakati akizungumza wakati akifungua Kikao Maalum cha Kwanza cha Kikundi Kazi cha Mapinduzi ya Kidijitali (Digital Transformation Working Group) cha TNBC, ukumbi wa TCRA, jijini Dar es Salaam, Tarehe 06 Novemba, 2023.
Viongozi wa Wizara, Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja na wadua wa TEHAMA wakaiwa katika Kikao Maalum cha Kwanza cha Kikundi Kazi cha Mapinduzi ya Kidijitali (Digital Transformation Working Group) cha TNBC, ukumbi wa TCRA, jijini Dar es Salaam, Tarehe 06 Novemba, 2023.
Katibu Mtendaji wa TNBC, Dkt. Godwil Wanga akizungumza wakati ufunguzi wa Kikao Maalum cha Kwanza cha Kikundi Kazi cha Mapinduzi ya Kidijitali (Digital Transformation Working Group) cha TNBC, ukumbi wa TCRA, jijini Dar es Salaam, Tarehe 06 Novemba, 2023.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha DTWG, Mohammed Khamis Abdulla akiwa pamoja na Mkuu wa Idara ya Kampuni ya Soft Net Technologies, Abdulrazak A. Seif wakati wakisaini mkataba wa kuchagiza mapinduzi va Kidijitali katika Kikao Maalum cha Kwanza cha Kikundi Kazi cha Mapinduzi ya Kidijitali (Digital Transformation Working Group) cha TBC, ukumbi wa TCRA, jijini Dares Salaam, Tarehe 06 Novemba, 2023.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha DTWG, Mohammed Khamis Abdulla(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Emerging Communication, Saidi A. Buhero wakati wakisaini mkataba wa kuchagiza mapinduzi ya Kidijitali katika Kikao Maalum cha Kwanza cha Kikundi Kazi cha Mapinduzi va Kidijitali (Digital Transformation Working Group) cha TBC, ukumbi wa TCRA, jijini Dar es Salaam, Tarehe 06 Novemba, 2023.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments