Ticker

6/recent/ticker-posts

Boy Cylla atwaa taji la “Rising Star Online Competition” la nPOINT Online TV

*Serikali yaonya wanamuziki kuhusu maadaili

Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Wakati Msanii Sailas (Boycylla) Mwakabana wa jijini, ameibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kwanza ya kusaka vipaji vya muziki ya Rising Star Online Competition, serikali imeonya wasanii ambao wanakiuka maadili ya Kitanzania.

Mwakabana ambaye ni msanii wa hip hop, ameibuka mshindi baada ya kuwashinda wasanii wawili waliongia fainali, Christian Job ambaye anatokea mkoani Iringa na Yusuph Hussein wa Dar es Salaam.

Mashindano hayo yaliandaliwa na kampuni ya N-Point awali yalishirikisha jumla ya wasanii 86 ambao walichujwa na jopo la majaji lililokuwa chini ya P-Funk Majani katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Radian ltd, benki ya Letshego Faidika, benki ya CRDB, FASTHUB, PrintPro, Tanzanie General, MMDT na Giraffe Hotel.

Kwa ushindi huo, Boy Cylla alizawadiwa zawadi yya Sh milioni moja taslimu na kupata nafasi ya kurekodi nyimbo zake za video, audio na gharama nyingine zenye thamani ya milioni 9 katika studio ya Bongo Records ya P-Funk.

“Nimefurahi sana kushinda nafasi ya kwanza, ushindani ulikuwa mkubwa sana, nawapongeza washiriki wenzangu wote kwa kuleta changamoto ambayo ilinifanya niongeze bidii na kuibuka mshindi,” alisema Cylla.

Kwa upande wale, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amewaonya wasanii wanao kiuka maadali ya Kitanzania na kurudisha nyuma sekta ya muziki nchini.

Msigwa alisema kuwa sekta ya muziki kwa sasa inakuwa kwa kasi na takwimu zinaonyesha kuwa zinachangia ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 19, lakini bado kuna wasanii wanakiuka maadili na kuwakimbiza wawekezaji.

“Unaweza kufanya vitendo vya ukiukwaji maadili jukwaani na kusifiwa na mashabiki wako, lakini baada ya muda, Baraza la Sanaa linachukua hatua dhidi yako kwa kukufungia, nani atapata hasara hapo, naomba wanamuziki mzingatie maadili..

Mbona marehemu Marijani nyimbo zake zinaimbwa wakati wote na vizazi tofauti na kutumia sanaa kuilinda nchi.

“Muziki ni biashara, muziki ni utamaduni, ni utambulisho na usalama, lazima tuuangalie muziki kimkakati na kutengeneza uchumi, ajira. Ni wajibu wa wanamuziki wanafanya kazi zinazotakiwa ili kuweza kufikia malengo,” alisema.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Radian Limited, Freddie Manento alisema kuwa wamefurahi sana kutoa fursa kwa vijana kushiriki na kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao.

Manento alisema kuwa shindano hilo litakuwa linafanyika kila mwaka na kuomba Basata kufanya marejeo ya gharama za kulipia vibali ili kuwapa fursa wakuzaji (mapromota) kuandaa matamasha mengi zaidi.

“Nawapongeza wadhamini mbalimbali kama benki ya CRDB,

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Basata, Kedmon Mapana aliipongeza nPOINT Online TV na wadhamini wakuu, Radian Limited kwa kupanua wigo wa matukio ya sanaaa nchini na sasa kufikia 77.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa (kulia) akimkabidhi zawadi ya ushindi wa kwanza msanii Sailas Mwakabana "Boy Cylla" katika mashindano ya muziki ya mtandaoni (Rising Star Online Competition) aliyofanyika kwenye ukumbi wa Msasani Tower jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya nPOINT Online TV. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Radian Limited, Friddie Manento. 
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa (kulia) katika pozi wakati mwakilishi wa benki ya CRDB, Rosemary Mashele (wa tatu kushoto) akimkabidhi hundi yenye thamani ya Sh milioni 5 mshindi wa kwanza wa mashindano ya muziki wa mtandaoni (Rising Star Online Music Competitions) msanii Sailas Mwakabana "Boy Cylla" (wa pili kulia). Mashindano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa Msasani Tower jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Radian Limited, Freddie Manento na wa pili kushoto ni Mwakilishi kutoka benki ya Letshego Faidika, Selestino Nachenga  kutoka benki ya Letshego Faidika.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa (kulia) akikabidhi cheti kwa mwakilishi wa benki ya Letshego Faidika Selestino Nachenga (wa pili kushoto) mara baada ya fainali za mashindano ya muziki wa mtandaoni (Rising Star Online Music Competition) yalifanyika kwenye ukumbi wa Msasani Tower. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Radian Limited, Freddie Manento
Mwakilishi kutoka benki ya Letshego Faidika, Selestino Nachenga (wa pili kushoto) akikabidhi mfano wa hundi  yenye thamani ya Sh milioni 5  kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya muziki wa mtandaoni (Rising Star Online Music Competition) msanii Sailas Mwakabana "Boy Cylla" (wa pili kulia). Mashindano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa Msasani Tower jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Radian Limited, Freddie Manento wakati wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa (kulia) akikabidhi cheti kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare (katikati) mara baada ya fainali za mashindano ya muziki wa mtandaoni (Rising Star Online Music Competition) yalifanyika kwenye ukumbi wa Msasani Tower. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Radian Limited, Freddie Manento
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya muziki wa mtandaoni (Rising Star Online Music Competition) msanii Sailas Mwakabana"Boy Cylla" (katikati) akishangilia mara baada ya kutangazwa kushinda mashindano hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Msasani Tower jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Radian Limited, Freddie Manento na kushoto ni mshindi wa pili, Christian Job.

Post a Comment

0 Comments