Ticker

6/recent/ticker-posts

FAO YAGAWA VIFAA VYA KISASA KWA BMU.

Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Merisia Mpalazo kulia akipokea moja ya vifaa kutoka kwa Mtaalamu wa Samaki FAO, Prisca Issangya. 
Diwani wa kata ya Moa Sitaruki Bwago akiongea wakati wa kikao.
Baadhi ya wanachama wa BMU wakisikiliza maelekezo ya matumizi ya vifaa hivyo.

*******************

Na Hamida Kamchalla, MKINGA.


SHIRIKA la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kupitia mradi wake wa limewezesha Vikundi vya ulinzi shirikishi wa bahari na Pwani (BMU) wilayani Mkinga kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vya uvuvi katika kuimaisha utekelezaji wao wanapokuwa kazini.


Wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi Wizara ya Mifugo, Merisia Mpalazo amesema Wizara inatekeleza maelekezo hayo kupitia sera ya Taifa ya uvuvi ya mwaka 2015, sheria za uvuvi, kanuni, miongozo pamoja na taratibu nyingine zilizopo.


"Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, pamoja na kutekeleza maelekezo hayo lakini bado tunatambua umuhimu wa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu yetu,


"Tukiwa sisi wenyewe hatuwezi kuyatekeleza ndiomaana tunashirikisa halmashauri za Wilaya, Taasisi zisizo za Kiserikali, Wadau wa maendeleo wakiwemo hawa wenzetu wa FAO, katika kuhakikisha kwamba tunafikia lengo la kufanya uvuvi uweze kuchangia kikamilifu pato la Taifa " amesema.


Aidha Mparazo amebainisha kwamba dhana ya ushirikishwaji huo inalena kuleta uwajibikaji wa pamoja wa wadau wote katika kuhifadhi, kulinda, kuendeleza na kusimamia rasilimali za uvuvi.


"Sote tunajua kwamba ushirikishwaji wa jamii ya uvuvi ni kupitia hivi vikundi vya rasilimali za wavuvi (BMU) ambao tunawatumoa sana na wanafanya kazi zao vizuri, na awa ndiyo wawakilishi wa wananchi wote walioko kwenye shuhuli za uvuvi" amebainisha.


Mtaalamu wa Samaki kutoka FAO, Prisca Issangya amesema lengo la mradi huo ni kuboresha usalama wa chakula, kuongeza ushiriki katika usimamizi wa matumizi ya rasilimali za bahari hususani kwa vijana na wanawake atika jamii za pwani.


"Lakini pia kuhimiza usimamizi wa uvuvi unaohusisha mfumo mzima ikiwemo uhusiano kati ya viumbe hai, makazi yao na muktadha wa mazingira kwa ujumla badala ya kuzingatia tuu viumbe vya baharini kama samaki unajumuisha vipengele vya ekolojia na jamii ya uvuvi ili kuhakikisha usimamizi unakua endelevu",


"Kupitia mradi huu vifaa kwa ajili ya kusaidia ufanisi wa usimamizi wa rasilimali bahari vitakabidhiwa kwa BMU ambavyo vitawawezesha kufanya misako na kukusanya takwimu lengo likiwa ni kuhimiza uchumi wa blue ulio endelevu" amesema.


Akiongea kwa niaba ya BMU na wananchi wa kata ya Moa, diwani wa kata hiyo Sitaruki Bwago ameishukuru shirika hilo kupitia serikali kwa kupata mradi huo ambao utaenda kuwaongezea ari ya ufanyaji wa shuhuli zao kwani uboreshaji uliofanywa ni mkubwa.


Amesema awali walikuwa na tatizo la vifaa duni ambavyo hawakuweza kufanya shuhuli zao ipasavyo lakini pia matukio ya kihalifu yalijitokeza kutokana na kukosa vifaa kama makoti ya majini, viona mbali, simu maalumu za mawasiliano baharini na vinginevyo ambavyo wamepatiwa.


"Tubaishukutu sana serikali yetu ya awamu ya sita, lakini pia FAO kwa kutuletea vifaa hivi ambavyo vitatufanya tuimarike kiutendaji katika shuhuli zetu za ulinzi wa bahari, lakini pia vifaa hivi vimekuja wakati muafaka ambao mahitaji yako kwq kiasi kibwa sana, tunashukuru sana" amesema.


Hata hivyo Bwago amewataka BMU kuvitunza na kuvitumia vifaa hivyo kwa matumizi yaliyokusudiwa ili viwaletee manufaa katika shuhuli zao ikiwa ni pamoja na kuwatua nguvu FAO kwa kuwaletea msaada huo kwani huenda wakapata moyo wa kuleta mradi mwengine katika Wilaya ya Mkinga.

Post a Comment

0 Comments