Ticker

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA SABABISHA TABASAMU YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TAASISI ya SABABISHA TABASAMU kupitia kauli mbiu ya isemayo "KISIMA CHA FURAHA" imetoa msaada wa nguo za watoto na mahitaji mengine mbalimbali kwa watoto na wenye mahitaji maalumu katika eneo la Mbopo Kata ya Madale Jijini Dar es Salaam yenye lengo la kupunguza hali mbaya iliyokithiri kwa wahitaji hao.
Akizungumza leo Desemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Bi. Adelina Ilomo amesema kuwa wameamua kuwasaidia watoto wa mtaani na wenye mahitaji maalumu kwasababu ni kundi ambalo limesahaulika.

Aidha Bi.Adelina amesema kuwa wananchi wanapaswa kushirikiana na serikali katika kuendelea kusiadia na kuziwezesha taasisi zinazojitoa kwa lengo la kugusa maisha ya watoto yatima na wahitaji waliopo mitaani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Mbopo Kata ya Madale Bw. Mohammed Bushiri amesema watu zaidi ya 40 wamefikiwa na kupatiwa mahitaji mbalimbali hususan nguo kwa watu wengi wasiojiweza.

Naye muhitaji kutoka maeneo ya Mbopo Bi. Mary Simon ameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia msaada huo hasa katika kipindi hiki ambacho wamekuwa na changamoto nyingi ikiwemo mavazi kwa watoto hao.

Post a Comment

0 Comments